JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Agostino Senga amesema uchunguzi wao kuhusu kifo cha aliyekuwa Mfamasia wa Kituo cha Afya cha Isansa, Wilayani Mbozi, Mkoani Songwe aliyetambulika kwa jina la Daudi Kwibuja (30) hakijatokana na ajari kama ilivyodhaniwa kutokana na mwili kuokotwa kando ya barabara Kuu itokayo Mbeya kwenda Tunduma katika eneo la Mlowo.
Amesema kuwa mwili wa mtumishi huyo wa idara ya afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi ulikutwa ukiwa na majereha mwilini mwake ambayo amedai kuwa katika uchunguzi wao majeraha hayo hayana viashiria vya ajali.
Akitoa taarifa ya kifo hicho, Kamanda, Senga, amesema kuwa wanaendelea na uchunguzi zaidi kubaini sababu halisi ya kifo hicho na kuchukua hatua kulingana ripoti ya uchunguzi wa kifo hicho kilichodaiwa kutokea usiku wa Julai 3, 2024.
“Uchunguzi unaendelea ili kuweza kubaini ni ajali kweli au mauaji, kwa hiyo tunaendelea kuchunguza na tutakapopata ukweli kupitia matabibu tutauhabarisha umma chanzo cha kifo cha ndugu yetu huyu (marehemu) kimetokana na nini ”, amesema Kamanda Senga.
Chanzo: Matukio Daima Media