Songwe: Mganga Mkuu wa Mkoa afafanua madai ya kusambaa kwa magonjwa ya tumbo na kipindupindu

Songwe: Mganga Mkuu wa Mkoa afafanua madai ya kusambaa kwa magonjwa ya tumbo na kipindupindu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Boniface Kasululu ametolea ufafanuzi taarifa ya Mwanachama wa JamiiForums.com aliyedai kuwa baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Songwe yana changamoto ya Wananchi kuumwa magonjwa ya matumbo na kuwa anahisi wengi wao wao wanasumbuliwa na Kipindupindu.

Kusoma andiko la Mwanachama huyo aliyedai baadhi ya maeneo yenye changamoto hiyo kuwa ni Kata ya Mpemba, bofya hapa ~ Kuna watu wanaumwa magonjwa ya tumbo/Kipindupindu maeneo tofauti ya Tunduma, lakini sijasikia tamko la Serikali

MAELEZO YA MGANGA MKUU
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Boniface Kasululu amezungumza na JamiiForums na kuelezea upande wake:

“Sina taarifa hizo za magonjwa ya Tumbo na Kipindupindu, sisi tunafanyia kazi hadi tetesi, nadhani Mdau angeweza kuweka wazi hizo taarifa za magonjwa zipo maeneo gani na hao wagonjwa wanapatikana wapi.

“Kuhusu Kata ya Mpemba aliyoitaja naomba nisitoe neno ili isije kuonekana nakataa kile alichokisema kama kina ukweli au la.

“Ujumbe wetu kwa Wananchi, siku zote tunatoa ujumbe kupitia redio na katika majukwaa na mikutano mbalimbali ya uongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na hata katika vikao vyetu sisi Mamlaka, tunakumbushana kuwa mtu yeyote mwenye dalili za aina hiyo inatakiwa kutolewa taarifa

Unaposema suala limefika kwenye Kata maana yake jamii inafahamu kinachoendelea, sitaki kupuuza kuhusu suala hilo, lakini kwa sasa kila mtaa kuna zahanati na zote zinashughulika na afya za Wananchi, kama taarifa hizo zipo na mimi sina taarifa ngoja nifuatilie.”
 
Hajazungumzia kukatika hovyo kwa umeme kunasababishwa na nini?
 
Huyu jamaa ni mewelewa sana hapendi kukurupuka na ni muwazi.

Ukikutana na wale wengine kwanza angekanusha hakuna kitu kama hicho na kuumalizia mama Samia hawezi kuruhusu watu wake waugue ovyo ovyo, maana serikali yake inapenda watu wake.
 
Back
Top Bottom