The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Wakati Serikali ikiendelea kuboresha miundo mbinu ya sekta ya elimu, uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe iliyopo mkoani Songwe, katika kuunga mkono jitihada hizo umetoa zawadi mbalimbali zikiwemo pikipiki, komputa mpakato (laptops), mashine za kunakili (photo copy mashine), kwa shule na walimu ambao wamesababisha ufaulu kupanda kwa madarasa ya mitihani ya taifa kwa shule za msingi na sekondari kwa mwaka wa masomo 2024.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo CPA Cecilia Kavishe, amesema wamekuja na ubunifu huo ukiwa na lengo la kuthamini mchango wa walimu pamoja na kuwapa motisha ya kufanya vizuri zaidi hasa katika sekta ya elimu ambapo halmashauri hiyo kwa kipindi cha miaka minne hali ya elimu imezidi kupanda huku walimu waliopata zawadi hizo wakipongeza ubunifu huo.