songwe: vivutio vya utalii vinavyopatikana halmashauri ya wilaya ya Momba na sifa zake

galimoshi

Member
Joined
Aug 5, 2023
Posts
11
Reaction score
8
picha .jpg
PIUVCCCCC.jpg

VIVUTIO VYA UTALII VINAVYOPATIKANA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOMBA NA SIFA ZAKE MKOANI SONGWE.

Momba ni kati ya wilaya Nne zinazo unda Mkoa wa Songwe, ambayo imebahatika kuwa na vivutio vingi vya utalii na vya kipekee hapa nchini Tanzania.

Licha ya upekee wake, vivutio hivyo bado vinahitaji msukumo wa Serikali na Jamii kuvitambua na kuvijengea mazingira rafiki ya kuvitangaza ili viweze kuleta tija na manufaa kwa uchumi wa nchi.

Vivutio hivyo ni kama vifuatavyo:

1. MAPOROMOKO YA MAJI MTO MOMBA (MPONA).

• Hili ni eneo la kipekee na la kuvutia ambalo pamoja na kwamba linaweza kuwa chanzo kizuri cha kufua umeme, lakini limejaa simulizi za kuvutia na kusisimua kutoka kwa wenyeji wa eneo hilo. Miongoni mwa simulizi hizo nipamoja na Maparomoko hayo kuwa na sifa ya kuwa na Nyoka mkubwa mwenye vichwa kumi na mbili ambaye anazungukwa na Njiwa weupe wasio kuwa na vichwa lakini wapo hai na wanaruka.

• Maporomoko hayo kwa waliofika wanaeleza kuwa ni eneo jembamba sana, ambalo kwa macho unaweza kutamani kuruka ili kwenda ng’ambo ya pili, lakini huwezi kufanya hivyo kwani unapotaka kuruka linajitanua na kuwa pana zaidi.

• Maporomoka hayo pia yanatoa tafsiri kwa wenyeji ya kujua musimu wa mvua upoje, aidha mvua nyingi, mvua za wasitani au mvua chache, kwahiyo eneo hilo pia linatumika kama mamlaka ya kutabili hali ya hewa kwa musimu husika.

• Simulizi zinaeleza kuwa Maporomoko hayo pia yanatumika kama eneo la tambiko kwa wenyeji hasa kipindi cha ukame mkali ili kuomba mvua, na mvua inanyesha kweli. Hizi zote ni simulizi za wazawa na endapo ukifika eneo husika unaweza kuambiwa vitu vingi sana kuhusu eneo hilo.

2. UNYAO WA MTU WA KALE.

• Unyao huo upo eneo la kata ya Nkangamo, ukifika eneo hilo utashuhudia unyao wa mtu wa kale ambaye alipita eneo hilo. Hiki ni moja kivutio cha kipekee ambacho kinapatikana ndani ya wilaya hiyo japo bado hakijatambuliwa na mamla husika.

3. TANURI LA KUFUA VYUMA.

• Tanuri la Kufua Vyuma ni moja ya mali kale ambayo inapatikana ndani ya jimbo la Momba. Tanuri hilo lilitumiwa na watu wa kale, kufua vyuma mbalimbali kama vile shoka, panga na mikuki kwalengo la kujilinda.

4. BWAWA LA MAJI LENYE KIVUTIO KIZURI.

• Bwawa hili linapatikana kata ya Ndalambo, upekee wake ni kwamba linamaji yasiyokauka msimu wote, maji yake ni masafi na yakuvutia machoni ambalo pia linafaa kwa uwekezaji wa kiwanda cha kuzalisha maji safi na salama kwa ajili ya matumizi.

5. JENGO LA KANISA LA KATOLIKI PAROKIA YA MKULWE

• Kwanza kwa umri kanisa hili lilijengwa na wamisionari miaka ya 1880s, kanisa hili kwa sasa linatimiza miaka 125 ya Uinjilishaji wa ukristo.

• Kanisa hili ndilo chimbuko la ukristo wakatoliki, Jimbo Kuu la Mbeya, sifa kubwa la Kanisa hilo ni kwamba limejengwa kwa ghorofa lisilokuwa na nondo na bado lipo imara tangu miaka hiyo.
6. NJIA ZA WATUMWA

• Hiki ni kivutio kingine amacho kipindi cha biashara za utumwa walipita njia hii katika kata ya Ikana na kwenda mataifa mbalimbali historia inaeleza hivyo.

7. SAFU ZA MILIMA YA UFIPA (UFIPA ESCAPMENT) NZOKA,NDALAMBO,CHITETE NA CHILULUMO.

• Hizi ni safu za milima ambazo ni moja ya kielelezo kubwa cha Jimbo la Momba, milima hii inatenganisha Momba ya Juu na chini, wenyeji wa eneo hilo ambao ni kabila la Wanyamwanga wanajina maarufu la (Kumkonde na Kumbo) –Kumkonde inamaanisha ukanda wa chini na –Kumbo inamaanisha ukanda wa Juu.

• Ukiwa ukanda wa Juu utashuhudia Bonde kubwa la Ufa na la Kuvutia na ukuwa Bondeni Utashuhudia safu nzuri ya milima ambayo imebabwa na miti aina ya Miyombo huku ukiburudiaka na maporomoko makubwa ya maji ya mto Momba wenyeji wanayaita AMPONA, ikiwa na maana ya anguko la maji kwa lugha ya wanyamwanga.

8. ENEO LA MSALABA WA KANISA KATOLIKI LENYE HISTORIA.

• Hili ni eneo lenye historia kubwa, kipindi cha ukoroni inakadiliwa miaka zaidi ya 100 iliyopita Wamisionari walikwenda kujenga msalaba mrefu juu ya mlima, iki ni moja ya kuinjilisha, mpaka leo msalaba huo unatumiwa na waumini wa wakristo kufanya hija, kwahiyo ni maja ya malikale ambazo zinahitaji kutambuliwa na kuwekwa kwenye kumbukumbu za kihistoria.

9. MADARAJA YA KITEPUTEP (SWEPENDED).

• Madaraja haya ya Kiteputepu pamoja na kwamba yanawasaidia wananchi kuvuka sehemu moja kwenda nyingine , lakini pia yamekuwa kivutio kwa watu wengi wanaofanikiwa kufika eneo hilo, hasa wageni ambao maeneo wanayoishi hawajawahi kushuhudia madaraja hayo.

• Madaraja haya ambayo yametengenezwa kwa mbao, nguzo na waya ni marefu wakati wa kuvuka yana nesa kama bebea za watoto, na kwa jimbo la Momba pekee kuna zaidi ya Viteputepu 10, ambavyo vingine vina histori yake. Kwamfano Kiteputepu cha Kamsamba –Chilyamatundu na kiteputepu cha Yala-Kanyala, vilijengwa na wamisionari zaidi ya miaka 100 iliyopita na mpaka sasa bado vinatumika.

10. MISTU YA HIFADHI YA ASILI

• Halmashauri ya Momba, imebahatika kuwa na hali ya hewa nzuri, na mistu aina anuai ya miti, ambayo inafaa kabisa kwa utalii. Kuna mistu mikubwa ya miti ya asili wenye uoto wa kuvutia. Kwa mfano mstu wa asili wa Ivuna, msitu wa asili wa Isalalo, mstu wa asili wa North ,mstu wa asili wa Chambo na mistu yote ambayo ipo safu ya mlima ufipa.

11. KUNA BIRD WATCHING-PINTAINLED HYDA, KING FISHER, COMMON BALBAL.

• Kata ya Chilulumo ndani ya wilaya hii ya Momba, kuna ndege wa kuvutia ambao sifa yake ni wapole na wenye rangi ya kuvutia, shingo ndefu, ndege hawa mara nyingi huonekana tu kipindi cha masika, wakati mvua zimeanza kunyesha, utafiti bado unafanyika inasemekana wanatokea bara la Asia.

12. FUKWE ZA ZIWA RUKWA.

• Momba ni moja kati ya Halmashauri tano za mkoa wa Songwe, ambayo imebahatika kuwa na fukwe nzuri mwambao mwa ziwa Rukwa, fukwe hizi ni za kipkee kwani kwa asilimia kubwa zimepambwa na nyasi za asili bala ya mchanga kama wengi wao walivyo zaoea, pia ina maji ya kipekee, unapobahatika kuyaoga yanasafisha sana mwili kutona na kuwa na sifa ya magadi wataalumu pia wanasema yanatibu magonjwa ya ngozi .

13. BWAWA LA CHUMVI –ITUMBULA.

• Bwawa hili la Chumvi lipo kijiji cha Itumbula kata ya Ivuna, hili ni moja ya bwawa ambalo lipo hapo tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia hii, na tangu enzi hizo lilitumiwa na wanchi kuchota maji na kuyagandisha kisha kupata chumvi ambayo ilitumiwa.

• Historia inaonyesha kwamba mikaka ya 80’s wazungu ambao walifika eneo hilo, walivutiwa na ubora wa chumvi iliyopo mahali hapo na kisha kutaka kuanza kuliendeleza, lakini hawakufanya hivyo baada ya miaka kadhaa kuhamisha makazi yao katika eneo hilo, baada ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu JuliusNyerere kufika Kata ya Ivuna na kutembelea maeneo hayo kuangalia raslimali za nchi.

• Pia kwenye Bwawa hili wenyeji wanatueleza kwamba, kwachini kuna mkundo wa mto mkubwa kutoka ziwa Tanganyika. Pia pembeni mwa bwawa hilo kuna kaburi la mtu mweupe (mzungu aliyefia kwenye mahali hapo alipotaka kufanya utafiti kwa kuzama kwenye kina kirefu na kisha kukutana na maji ya mato katika eneo hilo yaliyomuunguza na kupoteza maisha.

• Katika ufukwe wa bwawa hilo, pia utashuhudia mifupa na mafuvu ya wanyama wakubwa, ambayo mpaka sasa wakazi wa maeneo hayo bado hawajui hiyo ni mofupa ya wanyama gani, imebaki ni mashwali tu kwao; je ni mifupa ya binadamu wakale, au ni wanyama wa zamani? Maswahi haya mpaka sasa hayajapata majibu.

• Laki hivi karibuni Serikali imeiliingilia kati kwa kuanza kuboresha miundombinu ya bwawa hilo ili kuongeza kiwango cha uzalishaji na kuiongezea thamani chumvi hiyo ikiwa ni pamoja na kuiongezea madini joto, ingawa bado haijafikia malengo Kwahiyo bwawa hili la Chumvi litabaki kuwa malikale muhimu sana kutokana na umri wake na jinsi wazungu walivyo vutiwa na rasmali hiyo.

14. UTAWALA WA MACHIFU NA UHAI WA MABARAZA YAO.

• Kabila la Wanyamwanga ni kati ya Makabila hapa nchini, ambayo bado yanaamini sana mila na desturi za kichifu, kwa mfano kabila hili linaogonzwa na ukoo wa kichifu Mkoma (Siyame) ambaye pia ana kuwa ni mtawala wanchi mbili Tanzania na Zambia.

• Kabila la Wanyamwanga lina mila na desturi zake, hasa katika kuendesha sherehe za kitamaduni, wanakuwa na vyakula vyao vya asili, mavazi ya asili na hata malazi yao, wengi wao mpa sasa bado wanatumia vitanda vya kutengeza vya magome ya miti na mikeka.

15. KUGUNDULIWA KWA RASLIMALI ADIMU YA GESI YA “HELIUM”.

• Momba katika bonde la Ziwa Rukwa kwenye vijiji vya kata za Ivuna, Mpapa na Kamsamba kumegunduliwa hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium.

• Watafiti kutoka Chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa kushirikiana na wataalamu wa madini kutoka Norway wamegudua uwepo wa wa takribani futi bilioni 54 za gesi hiyo.

• Utafiti wa wali umefanyika, na kuonyesha matokeo makubwa, na kwa sasa utafiti wa awamu ya pili tayari nao umekamilika katika eneo hilo, amabpo tayari mitambo ya chimbimba visima imefungwa hapo. Kwahiyo ni moja raslimali muhimu katika taifa hili.

16. NGOME YA MALKIA.

• Ukifanikiwa kufika kata ya Mkulwe ndani ya wilaya hii ya Momba, wenyeji wanasema historia inaonyesha kuwa karne ya 19 kuna ngome ambayo Malkia wa Uingereza Elizabeth( I) alifika eneo hilo la kanisa katoliki Mkulwe na kuweka ngome yake ambayo mpaka sasa ukifika eneo hilo utaikuta, kwahiyo ni moja ya malikale ambazo wanachi wanatamu ziingizwe kwenye sera kwaajili ya uendelezaji.

17. MAPANGO YALIYOKALIWA NA WAKORONI KATA YA KAPELE.

• Ukifika kijiji cha Iyendwe kata ya Kapele ndani ya halmashauri ya Momba, wenyeji wa eneo hilo wanasimulia kwamba wakati wakoroni wanapita eneo hilo, walijiwekea hifadhi ya kuhishi kaatika mapango, na ukifanikiwa kufika eneo hilo, wakoroni hao walipanda baadhi ya miti ya matunda kama Miembe ambayo imesalia kuwa alama mpaka leo, kwahiyo ni moja ya maeneo muhimu katika fursa za utalii ndani ya wilaya hii.

18. UTALII WA KILIMO (AGRI-TOURISM)

• Utalii wa kilimo ni aina ya utalii wa mafunzo ambao umezoeleka kwenye mataifa yalioendelea Ulaya, Asia, America na baadhi ya nchi za hapa Afrika.

• Utalii huu uhusisha watalii kwenda kujifunza kile kinachofanywa kwa nadharia na vitendo kwenye mashamaba wanayoenda kutalii ili kujiongezea maarifa, ujuzi na ari katika kilimo.

• Momba ni Halmashauri ambayoama hakika imebahatikiwa kuwa na mashamba makubwa ya kilimo, ambayo pia yanafaa kabisa kwa utalii wa kilimo. Nikwamba ardhi yake inasitawisha mazao mbalimbali kama vile Mpunga, Maharage, Mahindi, Ufuta, Ulezi ,Alizeti n.k

• Umuhimu wa utalii wa kilimo ni pamoja na kuongeza maarifa na weledi katika kilimo cha mazao ya aina mbalimbli.

19. KIMONDO CHA IVUNA (THE IVUNA METEORITE)

• Mwishoni mwa mwaka 1938 historia inaonyesha kuwa katika eneo la Ivuna Tarafa ya Kamsamba kulidondoka na Kimondo (Meteorite) chenye ukubwa wa kilogram 0.7 kutoka angani.

• Hata hivyo Makumbusho ya historia ya asili (NHM) huko London wamenunua kielelezo kikubwa zaidi cha Kimondo cha Ivuna kutoka kwa mtu binafsi nchini Marekani

• Kimondo cha Ivuna nimojawapo ya Vimondo tisa tu vinavyojulikana ambavyo vimeainishwa duniani kama chondrites za kaboni , hidrojeni na heliamu karibu na kwenye juma kwa maana ya kwamba mimsingi havijabadilishwa kwa vile viliundwa karibu wakati ule ule na mfumo wa jua

• Kwa sasa Kimodo hicho kuna baadhi ya vinde vipo Mamlaka ya kusimamia miradi ya Serikali ya Marekani ya kuendesha utafiti na uchunguzi wa anga , National Aeronautics and Space Administration”

NB: Halmashauri hii ya Momba, imebahatakia kuwa na vivutio na malikale nyingi sana, ambavyo ama hakika bado havijawekewa mkazo kutambuliwa na kwewekwa kwenye kumbukumbu. Na vivutio hivi 19 ambavyo nimeviainisha hapa ni kwauchache tu, kwani ukibahatika kukaa na wenyeji wa eneo hilo wanabainsha vitu vingi ambavyo kimantiki vilipashwa kutambuliwa na mamlaka husika na kuingizwa kwenye historia.

Lakini bado hatujachelewa kwani wakati ni sasa wa kuweka msukumo zaidi wa kuanza kuvitambua na kuviwekea mkakati mathubuti.

Imeandaliwa na Laudens Lukas Simkonda-@Mwanahabari.

laudencesimkonda@gmail.com
0759359478/0655359478
 
Mkuu tupicha sasa hatupo. Umeweka andiko linalohitaji msaada wa picha ili liwe bomba zaidi. Sindikiza picha za kutosha mkuu
 
a.

• Maporomoko hayo kwa waliofika wanaeleza kuwa ni eneo jembamba sana, ambalo kwa macho unaweza kutamani kuruka ili kwenda ng’ambo ya pili, lakini huwezi kufanya hivyo kwani unapotaka kuruka linajitanua na kuwa pana zaidi.
Hii ni sumulizi ya MTO Kiwira kule kwa Wamanyafu
 
View attachment 3187006View attachment 3187008

Huko mnayapenda sana majina ya Lucas, kuna kivutio kipya hukohuko kinaitwa Lucas Mwashambwa zombie la kijani
 
Back
Top Bottom