Songwe: Waliokopa asilimia 10 na kutoroka kuanza kusakwa

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Vikundi 126 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, iliyopo mkoani Songwe, vimepokea mikopo ya 10% kutoka mapato ya ndani ya halmashauri hiyo awamu ya kwanza kiasi cha shilingi bilioni moja milioni mia mbili tisini na nane .

Soma Pia: Waziri Mchengerwa: Fedha za mikopo za asilimia 10 ni za moto, tusisikie vikundi hewa

Akikabidhi mikopo hiyo mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Bw. Hamadi Mbega, kando na kuishukuru serikali kwa kurejesha mikopo hiyo ametoa miezi mitatu nakuvitaka vikundi vilivyokopa kuanzia mwaka 2015-2023 na kutoroka na mikopo hiyo kujisalimisha kabla oparesheni ya kuwasaka na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ambapo mpaka sasa kiasi cha shilingi milioni mia tano na nne bado hazijarejeshwa.

bongo ndio sehemu mtu anakopa ili asilipe

KAZI KWELI KWELI/JOB TRUETRUE
 
Ninachojua pesa hzo sku hz wanapewa makada wa ccm tu
 
Fedha zinazoibiwa na kutoroshwa ni nyingi kuliko hiyo mikopo!
Vijana CHUKUENI CHENU MAPEMA( CCM)
 
Kama hiyo wilaya inaweza kukusanya B ya kutoa mikopo. Na bado inakusanya ya kutosha kuendesha shughuli zake hiyo sasa ndiyo wilaya ya kwenda kutafuta maisha
 
Vikundi 126 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, iliyopo mkoani Songwe, vimepokea mikopo ya 10% kutoka mapato ya ndani ya halmashauri hiyo awamu ya kwanza kiasi cha shilingi bilioni moja milioni mia mbili tisini na nane .

Soma Pia: Waziri Mchengerwa: Fedha za mikopo za asilimia 10 ni za moto, tusisikie vikundi hewa

Akikabidhi mikopo hiyo mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Bw. Hamadi Mbega, kando na kuishukuru serikali kwa kurejesha mikopo hiyo ametoa miezi mitatu nakuvitaka vikundi vilivyokopa kuanzia mwaka 2015-2023 na kutoroka na mikopo hiyo kujisalimisha kabla oparesheni ya kuwasaka na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ambapo mpaka sasa kiasi cha shilingi milioni mia tano na nne bado hazijarejeshwa.

Nimewasikia baadhi wakishukuru kuwa wameweza kuwalipia ada watoto wao, sasa huo mkopo wataulipaje!
 
Back
Top Bottom