Vikundi 126 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, iliyopo mkoani Songwe, vimepokea mikopo ya 10% kutoka mapato ya ndani ya halmashauri hiyo awamu ya kwanza kiasi cha shilingi bilioni moja milioni mia mbili tisini na nane .
Akikabidhi mikopo hiyo mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Bw. Hamadi Mbega, kando na kuishukuru serikali kwa kurejesha mikopo hiyo ametoa miezi mitatu nakuvitaka vikundi vilivyokopa kuanzia mwaka 2015-2023 na kutoroka na mikopo hiyo kujisalimisha kabla oparesheni ya kuwasaka na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ambapo mpaka sasa kiasi cha shilingi milioni mia tano na nne bado hazijarejeshwa.
Kama hiyo wilaya inaweza kukusanya B ya kutoa mikopo. Na bado inakusanya ya kutosha kuendesha shughuli zake hiyo sasa ndiyo wilaya ya kwenda kutafuta maisha