Sonso ameacha maandishi ukutani, tujitafakari

Nadhani TFF wangeweka kanuni kwa vilabu vyote vya ligi kuu kuhakikisha wachezaji wote walio sajiliwa wanakuwa na Bima ya Afya ya daraja kama lile la wafanyakazi wa Serikali.

Pia tuendelee kuwekeza kwenye Academy kwa vijana, ili tupate wachezaji walio kamilika. Badala ya kuendelea kuwakumbatia wachezaji wanao amini mpaka leo katika kupigana misumari, na pia bangi kama 'booster'.
 
Haya maelezo yoote yalikuwa yaandikwe paragraph moja tuu.
 
lakini Sonso si alifariki akiwa anapata matbabu Muhimbili?
 
Kama kuna mtu aliuona ule mguu wa sonso,ni dhahiri hiyo ni kansa

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Nimeona Ile picha mdau mguu umelika kabisaa Ila wanadai alitupiwa jini.......chanzo ni kugombea namba ya moja kwa moja pale ruvu na ni yeye mwenyewe ndio alianzisha hii Vita kumloga yule beki jamaa akaona isiwe tabu kama yeye kaanza mie namaliza.......sonso kaanzisha Vita kumbe Kinga Hana ndio yakamkuta yale
 
aliye mpiga misumari huyu dogo Mungu anamuona, hata akiokoka hili la sonso ataenda nalo adi kaburini, otherwise akaiombee msamaha familia ya sonso………….
 
Asante mleta mada umegusa kitu muhimu sana bima ya afya kwa wachezaji. Kama kumbukumbu zangu zipo vizuri miaka michache iliyopita TFF ilianzisha suala la bima ya afya kwa wachezaji na timu zililazimishwa kuwakatia bima ya afya wachezaji wao wote. Na walienda mbali zaidi kwa kuvilazimisha vilabu vikate hiyo bima vinginevyo visingeruhusiwa kushiriki ligi. Sijui huo mpango uliishiia wapi. Suala la Mudamu wa Polisi liwe funzo kubwa kwenye hili.

Hivi kweli kama TFF inaweza kuvilazimisha vilabu kuwa na timu za vijana ili ziruhusiwe kushiriki ligi kuu inashindwa nini kuvilazimisha hivi vilabu kukata bima kwa wachezaji wote . Na klabu itakayoshindwa kuwakatia bima wachezaji wake wasitoe leseni ya kuwaruhusu wacheze.

Vipi nayo makampuni ya bima na mabenki mbona yamekaa kimya kwa wachezaji wa mpira lakini yote yamejikita kwenye bima za mazishi au kutoa bima kwa wacheza mpira sio biashara nzuri kwao?

Ombi langu kwa vilabu vyote vijikite kutoa elimu kwa wachezaji wetu waache kuamini ushirikina hata kwa mambo yanayo hitaji matibabu ya kawaida hospitali. Vijana wengi wanatoka na imani zao kwenye hivi vilabu vya chini ambavyo vinaamini sana ushirikina wanafika kwenye vilabu vikubwa badala ya kuelimishwa wanakuta hata vilabu vikubwa navyo vimebobea kwenye ushirikina. Matokeo yake mchezaji akiumia kidogo tu au akipata changamoto yoyote mbio kwa waganga. Japo kifo ni mpango wa mwenyezi Mungu lakini huenda Ally Sonso angepata taarifa sahihi akabaki Muhimbili hali isingekuwa kuwa kama ilivyo leo hatupo naye.

Na viongozi wa vilabu nao wajitathmini. Nikiangalia suala la Sonso lilivyoshughulikiwa na viongozi wa timu yake naona kuna shida mahali. Hivi kiongozi unashindwaje kumfuatilia mchezaji kwa karibu tangu Novemba mwaka jana mpaka hali inakuwa mbaya Februari mwaka huu? Naamini kungekuwa na ufuatiliaji wa karibu viongozi wangejua mapema Sonso anapatiwa matibabu yasiyo rasmi wapi na wangegundua mapema kuwa matibabu anayopata sio sahihih na ingekuwa rahisi kumrudisha kwenye matibabu sahihi kwa wakati muafaka.
 
Piga picha huo ukuta aliouandika maelezo mbona mengi muda mchache
 
Ushirikina ni janga. Tumebobea kwenye ushirikina na unaturudi vibaya sana
 
Kua na bima ya afya hakuzuii ndugu wenye imani za kishirikina kukupeleka vilingeni
 
Bima Ya afya tsh 54000/= kwa mwaka
Mchezaji anashindwaje kulipa?
Uelewa mdogo tu
Yupo raisi mmoja kwenye nchi moja huko EA. alishawahi kuwaminisha watu wake kwamba dawa ya CORONA ni nyungu na maombi
 
Hujawahi kutana na ulozi broo, Sonso arogwa
Kama hosp Muhimbili walisema ugonjwa hauonekani kqbisa yaani yeye ni mzima ili hali yeye maumivu yanaendelea basi yawezekana tungewaelewa hao mandugu kumtoa hosp.
 
I see..ule mguu ulipata shida kubwa Sana..Kama Ni uchawi basi Kuna watu wanajua kuroga..Kama sio..basi Ni kansa Kama mdau alivyosema hapo juu..
 
Bima Ya afya tsh 54000/= kwa mwaka
Mchezaji anashindwaje kulipa?
Uelewa mdogo tu
Yupo raisi mmoja kwenye nchi moja huko EA. alishawahi kuwaminisha watu wake kwamba dawa ya CORONA ni nyungu na maombi
Hiyo ni gharama ya bima kwa watoto chini ya umri wa miaka 5 na bima inayotolewa vyuoni.

Pia ni 50,400
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…