Asante babu DC, haya mambo ya hisia bila jua ukweli mi wala huwa hayaniingii.
Kuna mwingine mtu alisafiri wiki bila kuaga akadhani ni alshabab kumbe wala hata sio ila kuna coincidence ziliingiliana hapo akajua alshaba kabsa
Ushauri wangu mwingine (Plan B) ikifika siku ya kwenda site na wewe jiandae, usimwambie kuwa unaenda. Akiingia kwenye gari na wewe tia timu. Mwambie leo honey nimejisikia ghafla kuandamana na wewe.
Afu mkifika huko mwambie naomba kutumia simu yako; hapo simu yako iache home sema umesahau. Hakikisha unakaa na simu ya Mr for as long as possible mwambie unachati na friend, ikibidi uwe unachati kweli hata na ndugu. Hapo ndo utaona huyo anayemzingua either anatuma message au anapiga. Utamjua mwizi wako. Kaba mama kaba mpaka penati.
Otherwise baki ila badili sim card yake kwa siku hiyo na kuweka new sim card na kuweka simu card yake kwenye simu yako but you need to save all his numbers in his phone book to that new sim card ili akitaka kumpigia asikwame afu set simu yake kwenye private number ili anayempigia asijejibu tumia new number ila atumie namba ya simu card uloiba(hii trick niliisoma humu humu JF)
Ngoja nikupe haka ka siri na mimi (wadada ipotezeeni kama hamjaona)
Mwanamke au mkeo akikupenda sana nao ni msalaba maana huwa inapelekea kitu kinchoitwa paranoia. Mme alichelewa tu unaanza kumuona anamvua nguo mwajuma. Afu labda mama ako anakupigia simu anakuambia mmeo kapita hapa kutusalimia basi wewe tabasamu linarudi usoni lakini kama usingeambiwa chochote utaona na lipstick kwenye kiatu chake.
Ndo mana mie husema kama mwanamke anaweza bora amwelewe tu mumewe.
Hajamshika na mwanamke zaidi ya kuhisi tu, chunguze kwanza hasa ndo mnapokuwa na mtoto mmoja huwa ni kama adolescence ya ndoa kwa wadada
We nyumba kubwa usimdanganye. Mwenzio ana mtoto mdogo na kwa stail yake ya kusimulia she is around mis twenties hicho kifua cha kukabiliana na reality hana.
Bi dada huyo kuku wako mwenyewe usimwinde kwa manati maana sidhani kama unataka kithibiti ili uvunje ndoa.
Sababu hajaongea naye bora aseme naye kwanza kwa hisani yake mwenyewe asisubiri miradi ya kimarekani
We nyumba kubwa usimdanganye. Mwenzio ana mtoto mdogo na kwa stail yake ya kusimulia she is around mis twenties hicho kifua cha kukabiliana na reality hana.
Bi dada huyo kuku wako mwenyewe usimwinde kwa manati maana sidhani kama unataka kithibiti ili uvunje ndoa.
Sababu hajaongea naye bora aseme naye kwanza kwa hisani yake mwenyewe asisubiri miradi ya kimarekani
Hakuna kitu ambacho sipendi kufanya kwa hubby wangu (toka ndoa ikiwa changa) kama kuongea bila facts. For sure ataishia kudanganywa na kugeuziwa kibao kuwa amezidi mawivu. Solution pekee ni kuwa na fact; end of story
Hamna cha kifua wala nini; yes atachanganyikiwa mwanzo but the truth will set both of them free.
Yaani uanze tu mume wangu nahisi una kimada; eeh ; hata mimi ningekuwa huyo mume nakutoa baru.
Ni kweli ila hiyo njia kama hiyo inawafaa akina Nyamayao,
Naamini bado anaweza kupata hizo facts bila kujiweka katika hatari ya kupata stroke..
Hatua ya kwanza ni kumdrill mume wako hadi kieleweke...Akishindwa hapo anaweza kurudi tumpe plan B ikiwemo hiyo uliyopendekeza wewe!!
Tatizo la hii mipango ya kando ni uchafu unaofanywa na watu wawili kumbuka.
Plan ya kumkaba mume inawork kwa masaa tu; akienda kwa kimada na kumwambia mke ameanza kunihisi lets stop kimada naye anaanza kumlilia hataki waache hako kamchezo. Na wanaume ni dhaifu; ataendelea tu as long as wife hana facts
Mi yashanikuta; nilihisi nyendo zimebadilika nikachimba bit. Hubby akamwambia kimada its over sitaki kuharibu ndoa yangu. Wacha kimada aanza kujiliza anasema bila yeye hamna haja ya kuendelea kuishi; ooh amebadili maisha yake;hajawahi kupendwa hivo maishani and lots of blah blah. Waliendelea mpaka nilipo pata evidence za kuua mtu ndo bidada akapigwa chini jumla.
Na tatizo ni kuwa nilivyochimba bit mwanzo nilikuwa nimehisi something lakini nilikuwa hata kumjua huyo "the other woman" Na hata baada ya kumjua ni mwanamke ambaye sijawahi kumjua maishani was the first time baada ya kujua jina through e mails ndo nika mtrace na kumuona kwa macho. Kwa kifupi niliingia kwenye private e mail ya hubby nikaona conversations zao zoote including ya bidada kuendelea kumganda jamaa baada ya kuambiwa ameamua kutulia na familia.
Mama haya mambo bado yapo ndani ya uwezo wako jitahidi kumrudisha katika hali ya awali kabla hajaanza hayo mambo naamini ukijichunguza wewe mwenyewe utagundua kuna sehemu uliikosea au uliidharau sasa inakuumiza MWANAUME ni kama mtoto kuna vitu alivipenda kwako na ndio maana akakuweka ndani jiulize alikupendea nini na sasa umebadilika nini
wakati mwingine wala mshkaji hafanyi kitu chochote, wanawake are good at imagining things hasa anapokuwa paranoid.
Paranoia ni ugonjwa mbaya sana unaweza ukaona sisimizi ukamkuza akawa tembo ukaita na game rangers waje wamuue.
sasa usiposema atajuaje kama hupendi hiyo tabia? Wanamme wanakamua nje lakini mwambie ili ajue abadili trick maana hiyo kama umeishtukia atumie nyingine ambayo haitakuumiza.
Acha kutumia antena tumia brain.