Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania wilaya ya Handeni Sophia Masimba amewataka makada wanaotarajia kugombea nafasi ya udiwani na ubunge na waliopo madarakani wilayani humo kuacha tabia ya kuchafuana kwa maneno kwa wajumbe ili kupata nafasi ya kugombea.
Akizungumza na wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Handeni kwenye muendelezo wa vikao vyao vya ujenzi wa nyumba za viongozi wa jumuiya hiyo menyekiti huyo amesema kuna tabia imeibuka ya makada kuanza kuwasema vibaya wenzao kwa wajumbe,kisa wanataka kugombea nafasi fulani.