Sophia Simba: Sigombei ng'o

Mchapaji

Member
Joined
Mar 22, 2010
Posts
26
Reaction score
1
Wadau, jana nilikuwa nikisikiliza kipindi cha JAHAZI, Clouds Fm na ndipo nikapata nafasi ya kumsikia Sophia Simba akihojiwa na Kibonde kuhusu swala la yeye kugombea mwaka huu....

Mama huyo alisema, hatagombea ubunge sehemu yoyote ile ila atakuwa mpiga debe tu kwa wanawake watakaojitokeza kugombea maana "piga ua garagaza" yeye ataendelea kuwa mbunge tu kutokana na wadhifa wake wa kuwa mwenyekiti wa baraza la akina mama...

Swali langu ni;
Hivyi uenyekiti wa UWT unaingilianaje na maswala ya kisiasa?
Ni vigezo gani vinatumika kumpa huyo mama ubunge bila kuutolea jasho?

Aksanteni.
 
Masihara haya sasa. Ninavyojua mimi ni kwamba VITI MAALUM vyiliweka kipindi kile kuwapa nafasi wanawake nao wawepo mjengoni maana wengi walikuwa wanashindwa kujitokeza kugombea lakini wengi wao ss wananguvu za kugombea.

Sofia Simba nilimsikia jana tena akisema wananchi wanampenda sana eti hata akitaka kugombea jimbo lolote hapa nchini atapita.... Jamani..............!!!!!!! Mhhh
 
Ni mwanamke jasiri mwenye kusimamia kauli zake tata na za kichovu..wanawake wanaweza lakini huyu Mmh!
 
Mbona wengi tu wanaingia huko bungeni bila kutoa jasho, kuna wale sijui wa kuteuliwa, kuna viti maalumu na kuna hawa wanaingia kiulaini kwa kutoa takrima badala ya jasho
 
Mbona wengi tu wanaingia huko bungeni bila kutoa jasho, kuna wale sijui wa kuteuliwa, kuna viti maalumu na kuna hawa wanaingia kiulaini kwa kutoa takrima badala ya jasho
Duh! hiyo ya takrima ndy issue...
 
Mjengoni kwenyewe wanafanya nini? Uzushi mtupu.!
 
"piga ua garagaza" yeye ataendelea kuwa mbunge tu
kwaiyo ni mbunge wa kudumu huyu au ila napenda ule ujike dume wake du
 
Ni mwanamke jasiri mwenye kusimamia kauli zake tata na za kichovu..wanawake wanaweza lakini huyu Mmh!

Kweli wanawake wanaweza lakini huyu huwa simuelewi kabsaaaaa, Kuna kinachomfanya ajiamini.
 
huyu mama ni kati ya viongozi ambao nni hazina kubwa sana ndani ya CCM, anafaa kuendelea na ubunge hata kama ni kupitia viti maalum na ninaamini ataendelea kuwa mbunge baada ya uchaguzi ujao
 
huyu mama ni kati ya viongozi ambao nni hazina kubwa sana ndani ya CCM, anafaa kuendelea na ubunge hata kama ni kupitia viti maalum na ninaamini ataendelea kuwa mbunge baada ya uchaguzi ujao
ZZZZzzzzzzzzzz???
 
huyu mama ni kati ya viongozi ambao nni hazina kubwa sana ndani ya CCM, anafaa kuendelea na ubunge hata kama ni kupitia viti maalum na ninaamini ataendelea kuwa mbunge baada ya uchaguzi ujao
Kama sisiem wana hazina kubwa ya viongozi kama huyu mama basi chama kimepotea!
 
Mbona wengi tu wanaingia huko bungeni bila kutoa jasho, kuna wale sijui wa kuteuliwa, kuna viti maalumu na kuna hawa wanaingia kiulaini kwa kutoa takrima badala ya jasho

Mbona ana uhakika huyu. Kwani nyie hamjui ni mmojawapo wa KAMLETE wa J.
 
Kiburi chake inawezekana napewa na mkuu wake wa kazi......., anawezaje kuwa na kiburi kiasi hichi huyu mwanamke? Lazima tu anabebwa na BOSS mkubwa!
 
TAYARI MIMI NI MBUNGE - SOPHIA SIMBA

Waziri katika ofisi ya Rais Mh. Sophia Simba amevunja ukimya kwa kuweka bayana kuwa hatagombea ubunge katika jimbo lolote lile hapa nchini Tanzania, kwasababu yeye tayari ni mbunge wa 2010 - 2015

Ningependa watanzania wajue kwamba mimi ni mbunge automatically, kutokana na nafasi yangu ya kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT
Na hii ni kutokana na utaratibu ambao chama chetu cha CCM umeuweka, ya kuwa Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti na Katibu wanakuwa ni wabunge tayari.

Pia amewataka wagombea wote (wanaume) kote nchini Tanzania wajue kuwa sasa moto umewaka. Kwasababu jimbo lolote ambalo mwanamke atajitokeza kugombea basi yeye atakuwa nyuma yao na kuhakikisha wanawake wanashinda.
 
Akili ya kivivu tu...kusubiri vya bure....halafu eti utawala bora sijui nini
 
Mpake hapo litakapotokea la kutokea wakampiga chini huo uenyekiti! Natamani angekumbuka ule usemi usiweke mayai yako yote kwenye kapu moja...ana "Plan B" just in case maana hizi kauli kama vile ajira yake ni ubunge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…