SORRY MADAM (52)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE……………………………
www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
‘Naogopa nini na mimi?’
Phidaya alijisemea kimoyo moyo. Akatoa woga
moyoni mwake kisha akaupeleka kwa kasi mkono
wake hadi kwenye kinyago cha Black Shadow,
akaufungua mkanda wa pili, kisha akaumalizia
mkanda wa tatu. Taratibu akaanza kukinyanyua
kinyago cha Black Shadow, asiye jitambua kwa
kupoteza fahamu, hadi kinyago hicho
akakitenganisha na sura yake. Moyo wake
ukampasuka baada ya kuiona sura ya Black
Shadow. Hofu ikamtawala, macho yakamtoka huku
akiwa amenata kama amegandishwa na sumanku,
kwa mbali akaanza kuhisi haja ndogo ikianza
kumwagika taratibu
ENDELEA
Kwa haraka Phidaya akakirudisha kinyago cha
Black Shadow kama kilivyo kuwa, akaanza
kutembea kwenda nje kwa vishindo. Kabla hata
hajafika mlangoni, akasikia mashine moja ikipiga
mlio, ikamlazimu kugeuka kwa haraka, macho yake
yakatua kwenye mashine inayo hesabu mapigo ya
moyo. Kwa kasi kubwa mapigo ya moyo ya Black
Shadow yakawa yanashuka.
“Mungu wangu?”
Phidaya alizungumza huku akijaribu kukiminya
kifua cha Black Shadow ili mapigo ya moyo
yasishuke, haikuwa kazi rahisi kwake, ikamlazimu
kuminya batani ya dharusa iliyo mtaarifu daktari
mkuu ofisini kwake, kwamba chumba alicho lazwa
Black Shadow kuna tatizo.
Haikupita hata dakika mbili Phidaya akasikia
mlango ukigongwa kwa nje, kwa haraka
akakimbilia kwenye mlango, wakaingia madaktari
wawili akiwemo na mume.
“Kumetokea nini?”
“Mapigo yake ya muyo yamebadilika gafla”
“Washa mashine”
Dokta Ranjiti aliwaamrisha wezake, kwahara
mashine ya umeme inayo tumika katika
kupandishia mapigo ya moyo ikawashwa. Kwa
haraka wakaanza kuigandamiza kifuani mwa Black
Shadow, na kukifanya kifua chake kustuka. Zoezi
hilo wakalifanya kwa dakika kadhaa pasipo
kuchoka, hadi inatimu mara ya ishirini na tano,
mapigo ya moy ya Black Shadow, yakarudi katika
hali yake ya kawaidia, kila mmoja akajikuta
akishusha pumzi ya wasiwasi.
Walipo hakikisha kwamba Black Shadow amerudi
katika hali yake ya kawaidia, wote wakatoka ndani
ya chumba, Phidaya na mume wake wakaelekea
ofisini.
“Baby kuna kitu nataka kukuambia”
Phidaya alizungumza mara baada ya kukaa kwenye
moja ya sofa lililopo ndani ya ofisi ya mume wake.
“Jamb……..”
Kabla Dokta Ranjiti hajamalizia sentesi yake simu
yake ya mezani ikaita ikabidia achukue mkonga wa
simu hiyo na kuiweka sikioni.
“Habari dokta Ranjiti”
Haikuwa ni sauti ngeni sana masikioni mwake.
Dokta Ranjiti akamtazama mke wake kwa macho
ya kuiba kisha akaiweka miwani yake sawa na
kuendelea kumsikiliza mtu aliye mpigia simu.
“Unatatizo gani?”
“Ohooo tatizo, unajua ni nini tatizo langu. Nahitaji
pesa, la sivyo nitamuambia kila kitu Phidaya
mwanamke unaye jifanya kumpenda”
Sauti hiyo ya kike ilimfanya dokta Ranjiti
kumwagika na kijijasho chembamba, hakuweza
kuzungumza jambo lolote mbele ya Phidaya. Woga
wake ulimfanya kuwa mtumwa wa siri kwa mtu
anaye mpigia simu.
“Unahitaji kiasi gani?”
“Ohooo hayo sasa ndio maneno. Najua hospitali
yako kwa sasa inakuingizia pesa nyingi sana.
Nahitaji dola milini moja, uiingize kwenye akauti
yangu ndani ya masaa kumi, la sivyo. Siri inakuwa
dirisha”
Simu hiyo ikakatwa na kumuacha dokta Ranjiti
akiwa katika hali ya mawazo, jambo hilo Phidaya
alilitambua kwamba simu iliyo pigwa imemkosesha
amani mume wake.
“Baby kuna tatizo?”
“Ahaa..ahaa hapana, nahitaji kwenda bank mara
moja”
“Kufanyaje usiku huu?”
“Ahaaa tutazungumza nikirudi”
Dokta Ranjita alizungumza huku akivua koti lake
jeupe na kuvaa koti lake la suti, akachukua funguo
ya gari lake kwenye droo ya mezani mwake,
akampiga busu la mdomoni Phiday kisha
akaondoka na kumuacha mke wake akiwa
hajazungumza kitu alicho kuwa amekusudia
kuzungumza.
***
Macho ya Shamsa yakamshuhudia dokta Ranjiti
akitembea kwa kasi akitoka katika mlango wa
kuingilia hospitalini. Akamuwahi na
kumsimamisha.
“Sahamani dokta, hali ya black shadow
inaendeleaje?”
“Vizuri, ila samahani binti nina haraka nahitaji
kuondoka kunasehemu nawahi”
“Lini atapona dokta?”
“Endeleeni kukesha na kumuombea, samahani
nahitaji kuwahi binti”
Dokta Ranjiti hakuona sababu ya kuendelea
kuzungumza na Shamsa, akaelekea kwa haraka
kwenye maegesho ya magari, akaingia ndani ya
gari lake na kuondoka kwa kasi hadi baadhi ya
watu walikishangaa hicho kitendo.
Shamsa akatazama huku na kule, alipo ona hakuna
mtu anaye mfwatilia, akaanza kutembea kwa
haraka kuelekea ndani ya hospitali, moja kwa moja
akaanza kuchunguza ni chumba gani wanacho
badilishia nguo manesi. Haikumchukua muda
mwingi sana kukipata chumba hicho, akaingia na
kukuta hakina mtu zaidi ya madroo mengi yaliyo
jengwa vizui ndani ya chumba hicho na katika kila
droo kuna mlango na juu yake ukiwa umeandikwa
jina la nesi anaye husika na droo hiyo. Akaanza
kuvuta kitasa cha droo moja baada ya nyengine,
mbili za mwanzo akazikuta zikiwa zimefungwa, ila
ya tatu akakuta ikiwa haijafungwa, akaifungua na
kukuta magauni mawili ya nesi huyo mwenye jina
la Si Ngii. Akachomoa gauni moja na kulipimisha
kwa urefu wa mwili wake, kwa bahati nzuri
limeendana naye. Akazivua nguo zake alizo zivaa,
akalivaa gauni hilo haraka haraka. Nywele zake
ndefu alizo kuwa amezibana kwa nyuma,
akazifungua na kuzimwaga kwa chini, kwa bahati
nzuri ndani ya droo hiyo akaona miwani ya macho
akaichukua na kuivaa. Akazichukua nguo zake na
kuzisokomeza ndani ya droo hiyo. Akaanza
kutembea kueleka mlangoni mwa chumba hicho,
kabla hajafika, mlango ukafunguliwa, akaingia nesi
mmoja anaye onekana kuwa na haraka,
hawakusemeshana kitu zaidi ya kupishana huku
Shamsa kichwa chake akiwa amekielekeza chini.
Akaanza kutembea kwenye kordo ndefu, kuelekea
katika chumba alicho lazwa Black Shadow.
Hakutaka kuinyanyua sura yake juu, kwani alihofiwa
kustukiwa, akazidi kupiga hatua za haraka hadi
kwenye mlango wa kuingila katika chumba cha
wangojwa mahututi. Akashika kitasa cha mlango
huo taratibu akaanza kukishusha chini huku
akitazama kuli na kushoto kwake. Akausukuma
mlango na kuingia ndani, akaurudishia mlango
huo, akageuka na kumtazama Black Shadow,
akiwa amelala juu ya kitanda huku akiwa
amezungukwa na mashine kadhaa. Akaanza
kupiga hatua kuelekea kitandani, hata kabla
hajakifikia kitanda milio mingi ya risasi ikaanza
kusikika nje ya chumba hicho, huku ving’ora vya
hatari vya hospitalini hapo vikianza kulia kwa
nguvu jambo lililo mstua Shamsa na
kumuogopesha sana.
***
Kitendo cha Young Po,kushindwa kutetea taji lake,
kilizidi kumuumiza sana. Kwenye maisha yake
hakuwahi kutarajia kwamba itakuja kutokea siku
atakuja pigwa na mtu katika mapambano ya
ulingoni. Hasira na chuki zikazidi kumpanda kila
alipo utazama mkono wake ulio vunjwa na Black
Shadow.
‘Lazima nifanye kitu’
Young Po alizungumza huku macho yake yakiwa
kwenye Tv kubwa iliyomo ndani ya chumba alicho
lazwa kwenye moja ya hospitali. Alikuwa akitazama
taarifa, kwenye kitua cha Jtv, kilicho kuwa
kikitangaza kwamba siku inayo fwata raisi wa nchi
hiyo atakwenda kumtembelea Black Shadow,
mpiganaji aliye tokea kupendwa na watu wengi.
Wivu ukazidi kumtawala Young Po, kwa haraka
akachukua simu yake iliyopo mezani, akaminya
namba kadhaa kwenye simu, baada ya sekunde
thelathini simu hiyo ikapokelewa.
“Njooni hospitaki sasa hivi”
Young Po akakata simu, baada ya robo saa,
mwanaume mmoja na mwanamke mmoja
wakaingia ndani ya chumba chake. Akawapa
maelekezo ambayo anahitaji yaweze kutekelezwa
usiku huo. Vijana hao hawakua na swali kwani
walimeelewa kazi ambayo wamepewa na bosi wao
huyo. Wakatoka hospitalini moja kwa moja
wakaelekea kwenye makao yao, ambapo,
wakawaelekeza vijana wengine watatu ambao
waliwaacha katika nyumba yao. Mpango wa
kutafuta gari ya wagonjwa, ikaanza. Halikuchukua
muda mrefu sana ndani ya lisaa gari ya wagonjwa
ikaletwa kwenye nyumba yao.
Bunduki zao zilizo jaa risasi za kutosha
wakaziweka ndani ya gari hilo, wkila mmoja
akachomeka silaha ambayo alihisi kwamba
itamsaidia katika kazi hiyo. Wakavalia mavazi ya
udaktari, kisha safari ikaanza kuelekea katika
hospitali aliyo lazwa Black Shadow.
***
Phidaya baada ya mume wake kuondoka, hakuona
haja ya kuendelea kukaa kazini, akavua mavazi
yake ya kazi na kuvaa mavazi aliyo kuja nayo
asubuhi. Akilini mwake akawa anafikiria kuhusiana
na donge nono ambalo polisi walilitangaza kwa
mtu ambaye atatoa ushirikiano wa kukamatwa
muhalifu ajulikanaye kwa jina la Eddy.
‘Lazima nipate pesa hizi’
Alijisemea Phidaya huku akidhamiria kuzipata pesa
kwa kuwatarifu polisi kwamba mtu wanaye mtafuta
ndio huyo Black Shadow aliye lazwa kwenye
hospitali yao. Akaanza kutembea kwa haraka
kuelekea kwenye maegesho ya magari, Akaingia
kwenye gari lake aina ya Aud A4.
‘Hakuna haja ya Ranjiti kujua’
Phidaya alijisemea kimoyo moyo huku akiwasha
gari lake na kuanza kuondoka, getini akapishana
na gari ya wagonjwa ikiingia huku likiwa linapiga
ving’ora. Hakutaka kulifwatilia sana kwa sababu
wapo madaktari wengine ambao watashuhulika na
mgonjwa huyo aliye letwa. Akaingia barabarani na
kuanza kuongeza mwendo kasi wa gari lake
kuelekea katika kituo kimoja cha polisi kilichopo
karibu na hospitali yao.
Ikamchukua dakika kumi kufika katika kituo hicho,
ika kabla hajasimamisha gari lake nje ya kituo
hicho, gari zipatazo kumi za polisi zilianza kutoka
kwenye kituo hicho kwa mwendo wa kasi.
“Mmmm kuna nini?”
Phidaya alizungumza huku akisimamisha gari lake
pembeni akizipisha gari hizi za polisi zipite, zilipo
malizika akaliegesha gari lake kwenye maegesho
ya hapo kituo cha polisi. Akashuka, askari mmoja
wa kike alipo muona Phidaya akamkimbilia hadi
sehemu alipo.
“Madam upo salama?”
Askari huyo alizungumza huku akimshika mkono
Phidaya.
“Ndio nipo salama kwani kuna tatizo gani?”
“Ina maana huna taarifa kwamba hospitalini kwako
kuna uvamizi wa majambazi?”
“Nini…..!!!”
Phidaya akajikuta akimtumbulia macho askari
huyo.
“Hizo gari zilizo toka hapo zinaelekea hospitalini
kwako”
“Twende twende”
Phidaya alizungumza huku akikimbia kwenye gari
lake, huku askari huyo akimfwata kwa nyuma,
wakaingia kwenye gari na safari ya kurudi
hospitalini ikaanza tena kwa mwendo wa kasi
sana.
***
Majambazi hao walio agizwa na Young Po,
wakasimamisha gari lao karibu kabisa na mlango
wa kuingilia ndani ya hospitali, manesi wawili
wakatoka na kuwapokea madaktari hao walio mleta
mgonjwa mmoja aliye lazwa kwenye kitanda cha
matairi wakaanza kumkimbiza ndani pasipo
kufahamu kwamba hao si madaktari. Wakiwa
katikati ya kordo, manesi wakastukia, mgonjwa
wanaye msukuma kwenye hicho kitanda
akinyanyuka huku akiwa na bastola mbili mkononi
mwake.
Manesi hao katika kushangaa, mmoja wao akaona
usalama wake ni bora akimbie, risasi kadhaa
zikamuingia kwenye mwili wake. Milio hiyo ya
risasi ikawastua watu wote walio kuwa ndani na
nje ya hospitali. Watu walio kuja kumuombea
Black Shadow, wote wakajikuta wakianza
kutawanyika kila mmoja akijaribu kuiokoa roho
yake. Baadhi ya walinzi wa hospitali wakakimbila
kwenye eneo la tukio huku wakiwa na bunduki
zao. Majibizano ya risasi baina ya walinzi na
majambazi hao walio fika hospitalini kwa lengo la
kumuua Black Shadow, yakazidi kupamba moto.
Shamsa akafungua mlango wa chumba alichopo,
akachungulia nje, akashuhudia nesi mmoja akiwa
amelala chini, damu zikiwa zinamwagika, watu
walio valia kama madaktari wakazidi
kuwashambulia walinzi wanao pambana nao.
Mapigo ya moyo yakazidi kumuenda mbio Shamsa,
hakujua afanye nini kwa wakati huo. Hata kabla
hajafikiria kitu kingine, gafla mlango ukapigwa teke,
akaingia msichana aliye valia nguo za kinesi,
mkononi mwake akiwa ameshika bastola.
Shamsa hakuhitaji kufikiria mara mbili kwamba
huyo ni nani, Akarusha teke moja lililo tua mkononi
mwa msichana huyo wa kijapani. Bastola
ikaanguka pembeni, macho makalia ya msichana
huyo, yakampandisha Shamsa kuanzia chini hadi
juu, msichana huyo akaanza kurusha mateke
mazito yaliyo mfanya Shamsa kuanguka chini
sakafuni. Msichana huyo akaanza kupiga hatua za
kuifwata bastola yake ilipo anguka, hata kabla
hajaichukua Shamsa akajirusha na kuwahi
kumdaka mguu msichana huyo na kumuangusha
chini.
Msichana huyo akarusha teke moja la ambalo
Shamsa alilikwepa na kuvuta chini, wakaanza
kubingirishana chini, huku kila mmoja akijitahidi
kukaa juu ya mwenzake, ili amshushie makonde ya
kutosha.
Mbiringishano huo, ukawapeleka hadi kwenye moja
ya mashine, wakajigonga hapo na kuifanya
mashine hiyo kuanza kuyumba yumba na mwisho
ikaanguka chini. Binti huyo alipo muona Black
Shadow akiwa kitandani akajaribu kusimama ili
kufanya agizo alilo tumwa, ila hata kabla
hajamgusa Black Shadow, Shamsa akamvuta na
kumuweka chini, na kuendelea kumshindilia ngumi
nyingi za uso.
***
Majira ya saa nane usiku, Raisi Praygod akiwa
amejilaza kwenye sofa lililopo pembezoni mwa
kitanda alicho lala Rahab, hafla akahisi mtikisiko
kwenye kitanda cha Rahab, ikambidi kuyafumbua
macho yake. Akamkuta Rahab akiwa anajibiringisha
kitandani. Wasiwasi mwingi ukazidi kumtawala
Raisi Praygod Makuya, akasimama kwa woga. Gafla
Rahab akakaa kitako kitandani, akayafumbua
macho yake huku akihema, jasho jingi likimwagika.
“Rahab”
Raisi Praygod alimuuita Rahab, huku akirudi rudi
nyuma, Rahab aliendelea kumuangalia raisi
Praygod pasipo kumsemesha kitu cha aina yoyote.
Taratibu Rahab akaanza kushuka kitandani,
akasimama wima na kuanza kumsogelea Raisi
Praygod aliye anza kurudi nyuma, hadi akagota
ukutana, Rahab akazidi kumsogelea taratibu huku
akiendelea kumkazia macho.
***
Shamsa akazidi kumshindilia ngumi, msichana
huyo ambaye naye alizidi kujitahidi kumzungusha
Shamsa, hadi akafanikiwa kumuangusha chini,
akamkalia Shamsa tumboni, na yeye akaanza
kulipiza makonde ambayo Shamsa alipatia muda
mchache ulio pita. Wakaanza kubiringishana tena
wakiendelea sehemu ilipo angukia bastola. Binti
huyo, anaye onekana amefuzu mazoezi mengi ya
kupigana, akaendelea kumshushia ngumi zilizo
changanyikana na vibao Shamsa, aliye iona
bastola imelala pembezoni mwake.
Askari walio fika eneo la hospitali, wakaanza
kuwatoa watu katika eneo la hospitali, huku
wengine wakiizunguka hospitali kuhakikisha
kwamba hakuna jambazi ambaye anatoka nje ya
hospitali hiyo. Askari sita wakaingia ndani wakiwa
na bunduki zao, walitembea kwa tahadhari hadi
kwenye kordo ambapo waliwakuta walinzi wawili
wa askari wakimpa huduma ya kwanza mwenzao
aliye pigwa risasi. Majambazi wawili walipoteza
maisha na kubaki wawili kwenye kodro, wakiwa
wamejibanza. Mashambulinzi yakaanza upya huku
askari polisi wakishirikiana na walinzi wa
hospitalini wakaendelea kuwashambulia majambazi
hao walio jikuta wakizidiwa nguvu. Askari polisi
wakazidi kusonga mbele, kwa bahati mbaya
majambazi hao wakajikuta wakiishiwa na risasi.
Hapakuwa na jambo jengine la kujitetea zaidi ya
wao kujisalimisha kwa askari hao.
Askari hao wakawafunga pingu majambazi wote
wawili, wakiwa wanawamalizia kuwafunga pingu,
wakastushwa na mlio wa risasi ulio tokea kwenye
chumba kilicho andikwa ICU.
Askari wawili wakavamia ndani ya chumba hicho,
wakamkuta msichana mmoja akijizoa zoa
kunyanyuka, huku akiwa amemuua nesi mwenzie.
Aliye endelea kuvuja damu chini.
Askari hao wakamuamrisha nesi huyo muuaji
kunyoosha mikono yake juu. Nesi huyo hakuwa na
ubishi taratibu akanyanyua mikono yake juu, askari
mmoja akamsogelea na kumfunga pingu kwa
nyuma. Askari hao wakamtoa nesi huyo nje ya
chumba wakamjumuisha na majambazi wengine
wawili. Wakawatoa nje kabisa kwa ajili ya
kuwapeleka kituoni. Shamsa akajikuta akistuka
baada ya kumuona Phidaya akimfwata katika
sehemu alipo shikiliwa na polisi.
“Hawa ndio majambazi eheee?”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya ukali, askari
mmoja akamuitikia, Phidaya bila hata kujiuliza
mara mbili, akamzaba kofi Shamsa, aliye kuwa
akimshangaa, pasipo kuamini kwamba huyo ni
Phidaya au laa, kwa maana wamefanana kila kitu.
Ilibidi baadhi ya askari wamzuie Phidaya
asiendelea kuwashambulia majambazi hao walio
ivamia hospitali yake.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 53 YA SIMUHILI HII.