Soulja boy ahukumiwa kifungo cha miezi 8. Wezi wavamia nyumba yake akiwa jela

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532


Soulja Boy afungwa jela miezi nane, wezi nao wamtenda
Rapa Soulja Boy amehukumiwa kifungo cha miezi nane jela na siku 265 za kufanya kazi za jamii kwa kosa la kuvunja masharti ya kipindi cha matazamio.

Akiwa mahakamani Jana (Aprili 30), Jaji alimueleza rapa huyo kuwa alikuwa anafikiria kumfunga miaka miwili jela lakini ameshawishiwa na namna alivyoishi kwa siku 40 akiwa nyuma ya nondo hivi karibuni.

Soulja alikuwa anatumikia kipindi cha matazamio pamoja na kufanya kazi za umma kwa kosa la kukutwa na silaha ya moto kinyume cha sheria mwaka 2014. Jaji ameeleza kuwa imebainika hakufanya kazi za jamii kama alivyoelekezwa na kwamba alishirikiana na baadhi ya watu kughushi vielelezo vinavyoonesha kuwa alikamilisha adhabu hiyo.



Februari mwaka huu, Polisi walishtukiza nyumbani kwa Soulja walipokuwa wakifanya uchunguzi kuhusu tuhuma zilizotolewa na mpenzi wake aliyedai rapa huyo alimteka.
Katika ukaguzi wao, polisi walidai kukuta baadhi ya vifaa vya silaha za moto, hatua ambayo ilichochea ugumu wa kupata unafuu.

Wakati huohuo, majanga yameendelea kumuandama rapa huyo kwani alipokuwa jela ndani ya kipindi hiki, kwa mujibu wa TMZ, wezi walivamia nyumbani kwake Agoura Hills, Calif na kuiba pesa taslim $100,000 pamoja na vidani vyenye thamani ya $500,000.


Dar24
 
Kujifanya usela mwingi
Wanaenda majela
Kunawapotezea muda na fedha tu!

Ova
 
Ana muonekano wa kipunga watampa mambo tu
 
Jela zao zilivyo na ubabe mwingi, makalio yake nayaonea huruma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…