Sound Bars za JBL

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2014
Posts
4,051
Reaction score
12,954
Juzi kati hapa nilitaka kununua sound bar nzuri jamaa yangu akanishauri ninunue za JBL kua ni nzuri sana.

Katika kufanya window shopping hapa Dar nikaenda Mlimani city nikauliza bei nikaambiwa, kisha nikaenda maduka mengine yako Sinza na mengine online nikapata bei.

Sasa kabla sijaamua kununua nikaingia mtandaoni kuuliza Sound Bars nzuri kilichonisikitisha karibu page 10 nilizotembelea moja tu ndio nilikuta JBL imetajwa tena walitaja ile ya 5.1.

Page nyingine zote JBL haijatajwa, nyingi ni Sony, Samsung na majina mengine mageni kabisa sijawahi kutaona Sound Bar zinauzwa Dollar elfu 4 na kuendelea.

Bado najiuliza je Sound Bar za JBL ni low budget sound bar kama za Hisense nk ama ni nini?

Wataalam naomba mawazo yenu.

Nashukuru.
 
Brand ndogo kwa vile vile rate zinawekwa brand kubwa izo JBL labda uende nje Kama marekani ndo utakuta ziko onfire ila kibongo bongo uchumi bado Kuna jamaa niliona yake kawaida Ina speaker za kuunga yaani zipo tatu ila ndogo unachomeka kweny bar kila ukingo jmaa kaniambia kachukua 3mil .
Mkuu sijakataa bei, swali langu ni kwamba mbona site nyingi online hawazitaji kama sound bar nzuri. Kuna sound bar wameweka za zaidi ya milioni 10 lakini JBL hazipo.
 
Chukua JBL Sound Bar, utafurahia sana.

Jaribu kwenda kwenye maduka yenye sound bar za kampuni tofauti ikiwemk ya JBL wakutestie miziki yake utagundua JBL ni bora sana..

Mimi mwenyewe natumia JBL Sound Bar.
 
Chief ungeelekeza umenunua wapi na gharama yake pia utakuwa umesaidia sana
Bei zake zinacheza kuanzia laki 9 hadi 2.8mil. inategemea na wauzaji.

JBL 2.1 nadhani iko kwenye TZS. 0.9m.
JBL 5 1 hadi TZS. 1.6m.
JBL 9.1 hadi TZS. 2.6m.

Maduka yapo mengi, unaweza kucheki kwenye Instagram ukapata wanaouza hapa Tanzania.

 
Nina Sony Music System Shake X30 haifikii JBL 9.1.

JBL nimeunga kwenye TV, miziki ya video nasikiliziia kwenye JBL mpaka nafurahia.
Naona ni bonge la combination ila mi nataka twin towers na ila hiyo Sony shake x30 na Yale mataa yake plus jbl soundbar Kama ulaya ile appearance hatar!!!!
 
Kwa bongo Nyingi ni fake zinakuwa zimebandikwa jina tu JBL. Maana wafanyabiashara wa bongo wajanja wajanja. Bora ununue samsung ama sony maana ofisi zao zipo Tanzania
Na hao uliowataja wana service centre DSM. Ikiharibika, kama ni SONY unaipeleka tu kule barabara ya cocacola Mwenge, au kama ni SAMSUNG wapo Samora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…