Kwa uelewa wangu, kuna njia mbili za kuweza kukabiliana na deficit kwenye budget ya nchi; moja wapo ni kuongeza mapato ili kifidia hayo mapungufu na hiyo ndio kama hivyo nchi inaweza kukopa ndani au nje ya nchi na njia hizi zote zina athari na faida zake. Njia ya pili ya kukabiliana na mapungufu ni kupunguza matumizi ili yalingane na rasilimali tulizonazo ; hii njia ya pili ni more plausible kwa Tanzania kwasababu kuna matumizi mabaya mengi katika serikali na taasisi zetu ambayo yanaweza kuthibitiwa ili kubalance budget yetu. Kuthibitisha kuwa kuna matumizi mapaya ya rasilimali zetu; achilia safari zisizo na tija za viongozi na ununuzi wa magari ya fahari, lakini pia kuna swala la fedha nyingi kwenda kwenye halmashauri lakini hata hivyo shule hazina vitabu wala madawati, zahanati hazina dawa na barabara za vijijini hazipitiki ingawa kuna allocation kubwa sana katika budget!! Ninahakika badala ya nchi kwenda kukopa nje au kwa commercial banks ,budget yetu inaweza kuwa balanced kwa kuthibiti matumizi ya serikali iwapo viongozi watakuwa realistic na kuachana na utashi wa kisiasa!!