Soya: Chakula chenye kinga na tiba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363



Mpendwa msomaji. Bado tupo katika kudadavua faida za kiafya zitokanazo na chakula.

Leo, tutaizungumzia Soya ambayo ni maarufu sana nchini lakini kwa bahati mbaya wengi

hawajui kuwa ni chakula chenye tiba ndani yake.


Ajabu ya chakula hiki ni pale kinapompa nguvu mgonjwa haraka bila kujali aina ya

ugonjwa anaoumwa. Katika ulimwengu wa vyakula, kuna maajabu mengi katika kukitumia

chakula kama tiba na kinga ya maradhi.





Mwaka 1999, Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa nchini Marekani (UFDA),

iliwaruhusu wasindikaji wa vyakula kutangaza rasmi kuwa soya ni halali na sahihi kutumika

duniani kote kama tiba na kinga kwa maradhi ya moyo, yakiwemo shinikizo la damu, kiharusi n.k.


Kama vile haitoshi, taasisi nyingi za kupambana na kutibu maradhi ya saratani duniani zimekuwa zikihamasisha matumizi ya lishe ya soya kwa wagonjwa wa saratani za aina

mbalimbali baada ya kushuhudia nafuu wanayoipata wagonjwa kwa kutumia bidhaa za soya.

Lakini, wapo ambao ndoa zao zinalegalega kwa kukosa hamu ya ndoa. ‘Saponon’

ambayo imo katika soya ikitumika kwa wiki kadhaa tu hamu hurudi katika hali ya kawaida

kwa jinsia zote: wanaume na wanawake ‘Saponon’ huchachua homoni

zinazouchangamsha mwili na akili pia.


Ukiachana na faida hizo, zipo nyingine kama vile kutibu mzio (allergy) za aina zote,

hukarabati ngozi na hujaza madini ya ‘calcium’ na ‘boron’ kwenye mifupa na kutibu

maradhi ya maumivu ya viungo kwa wenye miili mikubwa, wajawazito na wazee pia.

Soya ina madhara yake pia isipotayarishwa ipasavyo. Soya ina chembechembe aina ya

‘purine’ ambazo zimejikita kwenye ngozi yake na zikiliwa, mwili wa binadamu huzigeuza

kuwa tindikali iitwayo ‘uric acids’ ambazo ndizo chanzo cha maradhi mengi yakiwemo ya

vifundo au ‘gout’, japo ‘uric acids’ hizo hutoka mwilini kupitia mkojo.


Ni vyema ikaeleweka kuwa kula mimea na nafaka ni sawa na kusafirisha madini kutoka

ardhini kwenda mwilini. Kitaalamu, unaweza usiipate soya bora kwa kuwa hutoka katika

aina tofauti za udongo wenye madini tofauti.


Hapo ningependa kukushauri kuwa kama kweli una nia ya dhati basi tumia soya iliyotoka

mikononi mwa wataalam ambao wameiandaa vema soya hiyo ikiwemo kuipitisha katika

mamlaka za udhibiti wa vyakula na madawa kama vile TBS na TFDA za hapa nchini

ambako huangalia kama hazina sumu zitokanazo na uchafuzi wa mazingira.


Soya inaweza kutumika kama kinywaji chepesi au kama uji au kwa kuchanganywa na

unga wa nafaka zingine na kutumika katika kuandaa vyakula vya iana mbalimbali

ukiwemo ugali. Hakikisha unapata unga wa soya ulioandaliwa vyema na kuutumia

utakavyo ili kuupa mwili wako kinga au kujipa nafuu ya haraka kama ni mgonjwa.

Tiba za vyakula ni nyingi kama tunavyoziona kupitia safu hii msomaji wangu. Nakuomba

usikose kila Jumanne kufuatilia makala haya ili tujikomboe kiafya kupitia milo sahihi

ambayo ndiyo tiba popote duniani
 

Attachments

  • Soya.jpg
    26.1 KB · Views: 641
Tiba ya ugonjwa wa moyo?nijuavyo mm ugonjwa unaoua watu weng sana dunian ni ugonjwa wa moyo,tena hasa ktk nch zilizoendelea,sasa si wangekua wanatumia hyo soya wapone kabisa?kumbe tiba ipo madaktar wa ulaya hawataki kuwapa wagonjwa au hawajui?
 
Tiba ya ugonjwa wa moyo?nijuavyo mm ugonjwa unaoua watu weng sana dunian ni ugonjwa wa moyo,tena hasa ktk nch zilizoendelea,sasa si wangekua wanatumia hyo soya wapone kabisa?kumbe tiba ipo madaktar wa ulaya hawataki kuwapa wagonjwa au hawajui?
Waswahili wanasema Palipo na Miti hakuna Wajenzi . sasa hao wazungu wakiwapa Soya ili watu wenye ugonjwa wa moyo wapone ni nani atatumia Vidonge vyenye Sumu? Amka wewe kijana bado ninakuona upo usingizini. Wazungu wametengeneza ugonjwa wa ukimwi na Dawa wanayo lakini hawataki kuitowa wanataka wapunguwe watu duniani ndio watatowa Dawa ya kutibu Ukimwi.
 
Ok sasa mkuu tueleze jinsi ya kuitengeneza iyo soya ili kuondoa sumu ya uric acid.
 
Soya ndo nini?ama maharage yote ni soya?

Kama wewe ni mchaga wa uru, soya wanaiita "marisawa" ni aina ya maharage, rangi yake kijani cha kung'aa, ikikauka ina rangi ya chai ya maziwa, ile sehemu ya kiini ina rangi nyeupe
 
oya ni soya na maharage ya soya ni aina ya maharage na haina uhusiano na soya ila soya ni ndogo ndogo kama jugumawe
 
Napenda sana kutumia soya lakini huwa inakuwa na kiharufu flani ambacho huwa sikipendi. Kuna njia ya kukata harufu hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…