angella nafaka zote kama maharage, mahindi, karanga, korosho nk zote zinasababisha kansa. sina nia ya kuwatisha watu ila ukweli ni kwamba kama nafaka itakuwa attached na aspergillus hii ni aina ya fungus ambayo huwa inatoa sumu iitwayo aflatoxin. sumu hii inasababisha kansa.
kinachoweza kufanya nafaka kupata hawa fungus ni kutokukauka vizuri wakati wa kuvunwa na ndio maana unashauriwa uchague vizuri kabla ya kuitumia. pia unapotaka kuzisaga hakikisha ni kavu kabisa kabla ya kusaga na baada anika unga sehem kavu na hakikisha unga huo hautumiki kwa muda mrefu. iwe ni kwakipindi kisichozidi wiki 2, tena ukiwa eneo kavu.