Namfundisha mwanangu kiswahili sasa kaniuliza hii spana inayofungua bolts nyingi tofauti inaitwaje? Jibu najua ni Spanna Malaya..lakini hili jina halijakaa sawa kwa mtoto mdogo, maana anaweza uliza Malaya maana yake nini?maana sidhani kama ni vizuri kumfundisha mtoto mdogo maana ya Malaya. Je; kuna jina mbadala la hilo?naona kama jina hili limekaa kama isivyo.
Sio ni spana ya kurekebishika? Halafu kama spana malaya ni lugha ya kwawaida basi utamweleza ya kwamba "malaya" ni kitu kinachorekebishika kupokea vitu vyenye ukubwa tofautitofauti.
Akikua na kuona upande mwingine ataelewa falsafa ndani yake, au la?