Matinel sasa tatizo lako umeshakandia mikoa mingine huwezi pata sasa tutakusaidiaje
Usije dhani dar ni kila kitu siku hizi utandawazi.
Arusha hakuna spear au kipuri cha mashine yeyote unaweza kosa
Kumbuka Arusha imepakana na Kenya Dar haijapakana na nchi yeyote
Ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi
Usione Dar ni kubwa ukadhani kila kitu kipo
Arusha kuna mitaa ukipita kila sehemu kulia kushota wanauza spare za magari
Kuna sehemu zamani Arusha ilikuwa inaitwa Crokoni sijui kama bado papo basi pale hata injini ya ndege ukitaka unaweza pata.
Ukiweka uzi usikatishe watu wengine tamaa hapa tunasaidiana
Ngoja wajuzi waje wakusaidie ndugu yangu