LGE2024 Special Thread: Hali ya Vituo vya Kujiandikisha kupiga Kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kwa Picha na Video

LGE2024 Special Thread: Hali ya Vituo vya Kujiandikisha kupiga Kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kwa Picha na Video

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000

Wakuu salama?

Zoezi la kujiandikisha limezinduliwa jana Oktoba 11 na Rais Samia, meona nianzishe uzi huu ili tushee picha na video za maeneo ambayo tunaenda kujiandikisha kupiga kura.

Kuona vituo vikoje, mazingira kwa ujumla yanaridhisha? Au mnaandikishwa chini ya mti🌚!

Ukiweka picha na video hakikisha unasema huko ni wapi tujue kama serikali imewajibika vilivyo au oya oya mradi zoezi liende.

PIA SOMA
- LGE2024 - Video: Waandikishaji wapiga kura Uchaguzi Serikali za Mitaa waanza kuandikisha kabla ya muda wala uwepo wa mawakala

- LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

- LGE2024 - Wakala wa CHADEMA, Jacob Emily adaiwa kuumizwa alipokua akizuia majina yaliyoletwa na watu wa CCM kuingizwa kwenye daftari la uandikishaji wapiga
 
Hiki ni kutuo cha kata ya Mbokomu - Moshi, ambako mwanzo kilikuwa kimewekwa nyumbani kwa mgombea wa CCM wa kitongoji.



Baada ya wananchi kuwasanua ndio kikahamishwa na kuwekwa maeneo haya

IMG_0018.jpeg
 
Mbona huweki vituo ambavyo haviko nyumbani??
 
Nini kinahitajika ili niweze kujiandikisha, kitambulisho cha Taifa au ile kadi ya mpiga kura? Au naenda tu mwenyewe wanaandika?
 
ajabu mawakala wa chadema huko kwenye kuandikisha wanakosa hata chakula cha mchana na maji ya kunywa ukitaka kuamini chadema ni watu wa hovyo
 
Hivi hili zoezi la kujiandikisha linafanyika mitandaoni - huko mitaani mbona kama watu hawajali chochote kuhusu mambo ya uchaguzi, yaani hata kuyazaungumzia husikii popote.
Ni kwamba watu wamekata tamaa au hawaoni maana na umuhimu??
 
Mm huku nilipo sijaona foleni zaidi ya waandikishaji tu wakiwa wana wanachati na simu zao
FB_IMG_17290874704007749.jpg
 
Back
Top Bottom