Mwizukulu wa Buganda
Member
- Nov 19, 2024
- 94
- 307
Freeman Aikael Mbowe
Freeman Aikael Mbowe, kiongozi mwenye msimamo thabiti na maono makubwa, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa mara ya kwanza mwaka 2004. Kwa takriban miaka 21, Mbowe aliongoza chama hicho kwa ujasiri na ustadi mkubwa, akifanya kazi bila kuchoka ili kuboresha siasa za upinzani na kuimarisha demokrasia nchini Tanzania. Uongozi wake ulijikita katika kujenga chama chenye mshikamano wa kitaifa huku akilenga kupigania haki, usawa, na uwajibikaji wa viongozi wa umma.
Hata hivyo, Januari 22, 2025, Freeman Mbowe alikabidhi kijiti kwa Tundu Lissu baada ya kushindwa kutetea nafasi yake.
Je, kama Mtanzania, ni mambo gani utayakumbuka kutoka kwa Freeman (FAM) katika utumishi wa CHADEMA kwa nafasi ya Mwenyekiti?
Pia soma
- Breaking News: - Pre GE2025 - Freeman Mbowe akubali kushindwa, awapongeza Lissu na Heche kwa ushindi