LGE2024 Special Thread: Maoni ya Wananchi na Taasisi juu ya Mwenendo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa baada ya matokeo kutangazwa

LGE2024 Special Thread: Maoni ya Wananchi na Taasisi juu ya Mwenendo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa baada ya matokeo kutangazwa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakuu,

Uzi huu ni maalum kwaajili ya maoni ya Waangalizi wa Uchaguzi pamoja ma Wananchi juu mwenendo mzima wa zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa baada ya Matokeo kutangazwa.

Kupata taarifa zote za matukio ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kila mkoa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Kupata matokeo ya jumla ya Uchaguzi ingia humu: LGE2024 - News Alert: - CCM yashinda 98.83% Wenyeviti Serikali za Mitaa

Karibuni

=============================

~ LGE2024 - Simiyu: Upigaji kura wasifiwa kwa kwenda kwa amani na utulivu
~ Chama cha MAKINI kimeipongeza TAMISEMI kwa kusimamia vizuri Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
~ LGE2024 Njombe: Maombi ya Viongozi wa Dini yatajwa kuchagiza Amani wakati wa Uchaguzi Serikali za Mitaa
~ LGE2024 Mbeya: CHAUMMA wafanya pati ya Ubwabwa baada ya Ushindi wa kiti 1 cha Uenyekiti wa Serikali za Mitaa
~ LGE2024 TLP: Uchaguzi ulikuwa wa Huru na Haki ila Wapinzani hatukujiandaa kama CCM
~ LGE2024 Katibu Mkuu NRA: Sasa hivi yamekuwa maigizo kila mtu anasema katekwa, Uchaguzi ulikuwa wa Huru na Haki
~ LGE2024 Arumeru: Wananchi wamkataa Mwenyekiti wao mpya wa CCM, inadaiwa kampiga rungu raia na kumvunja mkono
~ LGE2024 Taasisi ya FOTO: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulikuwa na Huru na Haki
~ LGE2024 Viongozi wa Dini na Siasa Tanga waridhishwa na Uchaguzi Serikali za Mitaa
~ LGE2024 Chama cha NLD chaipongeza CCM kwa Ushindi wa Kishindo Uchaguzi Serikali za mitaa
~ LGE2024 Zitto Kabwe: Tunataka kuhakikisha hatulalamiki tu bali tunachukua hatua tunakwenda mahakamani kufungua kesi 67
~ LGE2024 Arusha: CHADEMA wapinga matokeo uchaguzi serikali za mitaa
~ LGE2024 Dodoma: Katibu wa BAKWATA, Askofu wasema kuna watu hawaitakii mema Tanzania, wanasambaza habari potofu kuhusu uchaguzi
~LGE2024 Njombe: Rose Mayemba asema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulikuwa ni operesheni ya kuwashughulikia wapinzani
~
~
 
Wakuu,

Uzi huu ni maalum kwaajili ya maoni ya Waangalizi wa Uchaguzi pamoja ma Wananchi juu mwenendo mzima wa zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa baada ya Matokeo kutangazwa.

Kupata taarifa zote za matukio ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kila mkoa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Kupata matokeo ya jumla ya Uchaguzi ingia humu: LGE2024 - News Alert: - CCM yashinda 98.83% Wenyeviti Serikali za Mitaa

Karibuni
bandiko muhimu sana hili 。
thanks
P
 
Hakuna umasikini m'baya kama umasikini wa akili na mtu ambaye ni maskini wa akili hana tofauti na mtu au watu wenye umasikini wa akili hawana tofauti na wafu/mfu,kwa sababu mfu au wafu hawajui lolote.

Kipindi cha bwana yule ambaye kwa sasa hayupo katika dunia hii,kila baya lililo tokea alishutumiwa yeye kunajisi Katiba na chaguzi,kuhusishwa katika kupotea kwa watu na wengine kukutwa kwenye viroba na mengine mengi.Alipo itwa katika safari yake ya milele na nafasi kuchukuliwa na kaimu wake.

Nyimbo na mapambia pamoja na nyuzi za Kusifu na kuabudu hazikukatika katika majukwaa mbalimbali,watu wakaenda mbali zaidi na kubuni misemo mbalimbali kama "mama anaupiga mwingi","Chawa wa mama",Samia 5 tena" nk

Walidhani kwamba Kuna mageuzi ya kuona Mwanga,baada ya kiza na mapito katika bonde la mauti ,wakasahau kuwa kipindi cha mapito ya kiza na bonde la mauti,mtu yule waliye mtarajia kwamba analeta Mwanga alikuwa sehemu ya mfumo ule ule na ni sehemu ya mfumo huo,hivyo anaelewa kila jambo.

muda mfupi mfano kubadili jina la Tume ya uchaguzi,kuwatoa baadhi ya wateule wa bwana yule walio kuwa na shutuma mbalimbali kwenye nafasi zao,kuunda kikosi Kazi,kufanya mabadilko kiini macho kwenye sheria za uchaguzi(kupitia Bunge) zikiungwa mkono wa mahakama kipofu,kufuta kesi za kisiasa na maridhiano nk.

Wajinga na wapumbavu wakaingia mkenge sio nyama vya siasa,wanahabari,asasi za kiraia, viongozi wa dini,wasanii,wanamichezo nk

Wanahistoria wanamsemo wao huu "Historia ina asili ya kujirudia" ghafla yale yaliyokuwa yanatokea kipindi cha bwana yule yamerudi kwa njia ilele kutekwa,kupotea na kuuawa,wateule wenye shutuma kurudi kwenye nafasi na mengine mengi lakini watu wakajivika miwani za mbao ni wachache walio sema au kujua Kuna kiini macho tu na sio dhamira ya dhati ya kuleta mageuzi,waliopo paza sauti zao walipuuziwa.

Kituko cha funga mwaka ni 2024 kama ya 2019,ambapo kila mtu sasa anatoa matamko kama mwendawazimu huku wakisahau mtoto wa Nyoka ni Nyoka.

Sasa ni mwendo wa kusubili la 2025,kama litakuwa kama la 2020,tuwe na uzima kuona yajayo.Wafuasi wa bwana yule wanacheka jinsi mambo yalivyo badika ghafla na kuwa acha wenye matumaini kwenye kiza kinene.
 
Hahaha hat wao CCM wanatambua hawapendwi, lakini hawana jinsi, ilibidi kufanya walivyofanya kumfurahisha mwenyekiti yani SSH.
 
Back
Top Bottom