ii) KOMPRESA ZA KUJAZA UPEPO
katika kundi hili kikawaida kompresa ndgogo kabisa yenye uwezo wa kujaza upepo ni lita 50( hii itumike kwa pikipiki tu ) ila kwa upande wa pili ni kompressor za magari ambapo kitu kikubwa ambacho kinaangaliwa ni uwezo wa compresa , vitu kama ujazo wa mtungi , idadi ya piston pamoja na uwezo wa mota au ukubwa wa engine(HP) pia kitu kingine cha kuzingatia ni electrical installation ya eneo ambalo unafanyia kazi , kama ni single phase basi aina ya motor ambayo itakuwa kwenye kompresola yako hakikisha nayo iwe single phase (220-240v) vivyohivyo kwa 3 phase nayo hakikisha iwe 380v
Pia zingatia kama hakuna umeme basi itabidi uwe na kompresa inayotumia mafuta na kama kuna umeme unaweza ukawa na ya umeme pia , kwa maeneo ambayo ni korofi umeme unakata hovyo unaweza ukachukua 2 in 1 yani umeme pamoja na mafuta
Gharama za kompresa
Lita 50 (belt driven)>>650,000
Lita 100 (umeme)>>> 950,000
Lita 100 (mafuta)>> 1,150,000
Lita 150 (umeme)>>1,150,000
Lita 200 (umeme)>> 1,350,000
Lita 200 (2 in 1)>>>1,750,000
Lita 300 (umeme)>> 1,850,000
Lita 300 (2 in 1)>> 2,450,000
Lita 500 (umeme)>>3,300,000
Lita 500 (2 in 1)>> 4,500,000
Cha kuzingatia ni kwamba hizi compressor zinakuja zikiwa configured kutoka kiwandani , kwa mteja ambaye anaona angependa kuifanyia mabadiliko compressor yake inawezekana kwa mfano kompresa ya lita 200 kuibadilishia motor kutoka 3 hp hadi 5 hp na lia kubadilisha kichwa cha kompresa inawezekana kutoka 2 piston head hadi 3 piston head kulingana na mahitaji yako mteja
ANGALIZO, matatizo makubwa kwenye hizi compressor yanapatikana kutokana na uzembe wa operator kutozingatia uwekaji wa oil (aina pamoja na kubadilisha oil) tatizo hili upelekea uharibifu mkubwa sana kwenye piston za kompressor head na pia kwa compressor za umeme capacitor zinaungua sana kutokana na power surge
View attachment 2973516View attachment 2973518View attachment 2973519View attachment 2973520View attachment 2973521