Special Thread: The 2am/5am Club

Special Thread: The 2am/5am Club

Teslarati

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2019
Posts
2,621
Reaction score
10,466
Salute comrades,

Nimefikiria kuanzisha hii chat kwa wale tunaolala saa nane usiku(2 am) au kuamka saa kumi na moja alfajiri (5 am) sababu ya majukumu mbalimbali ili tuweze kushare vitu mbalimbali kama vile:

1) Tips za kuwa productive kazini.
2) Work-life-family balance.
3) Diets.
4) Life hacks.
5) Sehemu tulivu za starehe.
6) Vinywaji.
7) Kufahamiana.
8) Kupeana deals na michongo.

Na mambo mengine ya muhimu.

Nimefikiria kuanzisha hii kitu sababu December huwa ni mwezi wa likizo lakini nipo hapa town ila watu wamepoteza kabisa ule utamaduni wa kukutana na kushare mambo mbalimbali.

Nilikua nmezoea miezi hii tunakutana watu kama sita hivi au zaidi kushare mambo mbalimbali lakini wengi wamepotea kwenye machimbo tulozoea kukutana. Wengi tumekua kwenye media 24/7, so ni bora tutumie media kushirikishana mambo yatakayorahiisha maisha yetu.

Karibuni.
 
Kuna muda hasa hasa katikati ya saa tano asbh na saa saba mchana unaweza feel like shit. Yaan unakosa mood kabisa ya kufanya chochote kile unajisikia very anxious, kila unachogusa unaona hakiendi. Hii sababu kubwa ni kukosa simple sugar ya kutosha kwenye breakfast yako. Ubongo unakosa nguvu na unashindwa kufocus vzr.

Solution inabidi ujitahidi uwe na CHOCOLATE au fast food yoyote yenye sukari sukari ambayo unaweza kua unakula huku unaendelea na kazi zako, chagua task moja anza nayo kwa kujilazimisha huku unakula hicho kitu. Ukiforce kufanya hivo kwa dakika 5 basi automatically hio feeling ya kujisikia hovyo inaisha ghafla.

Hii njia nmetumia sana na inaleta positive results, try it and post feedback kwa manufaa ya wote.
 
Back
Top Bottom