KUPAKA RANGI
Utangulizi
Mara nyingi watu hutafuta mafundi kwa ajili ya kupanga rangi nyumba zao ama sehumu za nyumba zao na kuta za ua. Hii ni sawa kabisa kwani mafundi wanauzoefu na ujuzi unaohitajika katika upakaji rangi.
Lakini upakaji rangi ni jambo linaloweza kufanywa na mtu yeyote kama atazingatia jinsi ya kupaka rangi na hatua zake. Makala hii itahusika na upakaji wa rangi ya maji.
Mahitaji
1. Rangi ya maji
2. Brashi mbili ama brashi moja na rola
3. Skrepa/kikwanguzi
4. Msasa
5. Ndoo tupu
6. Maji
7. Kipande cha godoro ama kipande cha kitambaa
8. Selotepu na magazeti.
MATAYARISHO
Ni muhumi matayarisho yafanywe siku moja kabla ya kupaka rangi ili kuwezesha ukuta kukauka vizuri kama kiziba nyufa kilitumika. Pia hii usaidia vumbi kutuama ama kuelekea nje kupitia madirisha kutokana na mzunguko wa hewa.
Hatua ya kwanza ni kuvitoa nje vitu vinavyohamishika vilivyomo ndani ya eneo husika. Ama unaweza..
Vitu vyote vinavyohamishika vilivyomo ndani ya eneo husika au la unaweza kuvikusanyia katikati ya chumba na kisha kuvifunika kwa kitambaa ama nailoni. Hii itasaidia kukupa nafasi na eneo tosha la kufanyia kazi na pia vitu vyako na hasa samani havitachafuliwa na rangi.
Kumbuka kama hutaviacha vitu hivi ndani na hautavifunika pia utalazimika kuvisafisha badae! Upotezaji wa muda na nguvu usio wa lazima! Kama unahitajika kupanga rangi dari(ceiling) ambalo lilikuwa na rangi, tumia msasa kulisugua taratibu kuondoa chembechembe zisozogandamana. Kama unalipaka rangi dari lako kwa mara ya kwanza basi hamna haja ya kulisugua kwa kutumia msasa.
Baada ya kupiga msasa dari lako sasa piga msasa kuta zako kuondoa chembechembe zote zisogandamana na uchafu ama madoa. Baada ya zoezi hili tazama vizuri kuta zako kubaini nyufa ama mashimo. Kama kuna nyufa, au mashimo basi tumia kiziba nyufa kuyaziba.