Special Thread: Wauza TV aina zote kwa bei nzuri tuuziane hapa

Wakuu nitoeni ushamba kidogo (nataka kujifunza) eti nini tofauti kati ya Smart TV na LED TV?

Sent using Jamii Forums mobile app
Smart inaweza kuwa LED ila sio kila LED ni smart anyway ni hivi....
LED Ni aina ya technology iliyotumika kutengeneza kioo cha TV ambacho haili moto mwingi na huwa na kioo cheusi zaidi na kuna LCD na PLASMA hizi ni technologies za nyuma kidogo ambazo zilikuwa zinatumia aina ya bulb ili kuleta mwanga kwenye display pia kwa sasa kuna OLED na QLED ambazo ni latest technology za kioo cha TV na hufanya kioo kiwe chembamba zaidi hata kufikia mithili ya WEMBE.

UKIJA SMART TV ni aina ya mfumo endeshi wa TV yako sasa hapa kama unavoona kuna simu za kawaida na kuna smartphone na zaidi hizi SMART TV huipa uwezo TV yako kufanya mambo mbalimbali kama kuinstall APPs kwenye TV,Kustream Video kupitia sehemu kama YOUTUBE,NETFLIX,Kuchat FB,INSTA n.k kwa kutumia INTERNET aidha toka Kwenye Smartphone yako (WIFI) au kifaa chochote utakachotumia kushare hiyo NET.

Hiki ndicho nachoelewa mkuu ngoja manguli waje jazia na ninerekebisha pale nilipoteleza

PLASMA.
LCD.
LED.
OLED/QLED. kwa sasa
 
Mwenye tv kuanzia inch 40 LED brand yoyote nzuri na iwe slim nataka tufanye exchange na laptop yenye specs zifuatazo
Dell Latitude E7240
Core i5
Ram 4 GB
SSD 128
Very Portable and Slim
npo dar
 
hili ni somo zuri nimeshaelewa sasa hapa
 
Mwenye LED TV ya SONY,SAMSUNG naomba offer yako ma picha inch 28 au 32 Iwe USED au Anaeuza duka la TV USED za Nje.karibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…