LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
"Kila mzarau mwiba mguu huota tende". Putin hakutegemea kuhenyeshwa namna hii na nchi ambayo ni sawa na mkoa wake. Inasemekana ashaongeza idadi ya wanajeshi baada ya wale aliowatuma kuuwawa, kutekwa na kujeruhiwa vibaya, pia wameshindwa kufikia malengo waliyopanga. Walitarajia kumaliza vita kwa usiku mmoja, sasa leo ishakuwa week na matumaini ya kile wanachohitaji hayaonekani. Huenda akishindwa tena kukamata mji mkuu ataongeza tena jeshi na mwisho wa siku atajikuta yuko peke yake nchini, huku jeshi lake lote likiwa mapiganoni. Waswahili wanasema "vita vya panzi, ni furaha kwa kunguru". Najua sasa hivi Marekani wanacheka tu jinsi Mrusi anavyozidi kumaliza jeshi lake na silaha zake vitani. Watahakikisha mrusi anabaki hoi kijeshi na kiuchumi.
 
Japo namsaport Putin ila hii video inasikitisha sana mlemavu kaacha wheelchair [emoji174]huyo mtoto aliyevaa mask na baba ake aisee tuombe Hii vita iishe tu
We kama unaomba omba kipekeako..
Sidhani ka hao wazungu walishawai waombea watoto wa Libya, palestrina au Africa ...
Kila mtu alie kilio chake... ts non of our fckn bsnss
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] PRO-NATO
 
Vitendo vya kiharifu?? USA to Iraq, Libya Na Israel to parestina hivyo sio vitendo vya kiharifu???
Wewe una emotions tu hakuna unachojua, hufahamu kuwa ghadafi alituma jeshi na silaha Uganda kipindi cha ya kagera, umesahau Russia aliivamia afighanistan, hoja za kishabiki zipo kwetu ambapo watu wengi akili hamna hawafanyi analysis, unaweza ku analysis hii vita kwa jicho la ubinadamu, athari zake kwenye jamii zetu mpaka huku kwetu kwa wachambuzi
 
usitudangaye kijana sisi sio watoto kyiv imeshikwa vibaya rais wao analialia tuu.
 
Tuombe tu yaishe maana akizidiwa kwa kiwango unachosema atakuwa hana tena cha kupoteza. Sasa mtu ambaye hana tena cha kupoteza na ana silaha za maangamizi unadhani atachukua maamuzi gani? Unless ipo njia ya kumdhibiti asifanye mad decisions.
 
Vitendo vya kiharifu?? USA to Iraq, Libya Na Israel to parestina hivyo sio vitendo vya kiharifu???
Mwenzako nilimjibu hapa ila ni kama mko wengi, kwa hiyo Marekani kufanya uhalifu kunahalalisha Urusi na yeye kufanya uhalifu?
 
Mjumbe Ghana UN General Assembly : We call Russia to ceasefire and withdrawal of their troops in Ukraine, we suggest diplomatic ways to solve the problem
 
We kama unaomba omba kipekeako..
Sidhani ka hao wazungu walishawai waombea watoto wa Libya, palestrina au Africa ...
Kila mtu alie kilio chake... ts non of our fckn bsnss

Tatizo umekurupuka kujibu kuomba sio lazima kuwaombea wazungu kuomba vita iishe isije ikafika had huku tulipo ni shida kama NATO wakijibu anyway mf. Sasa mafuta yamepanda huko unadhani haitokuja kutuathiri nasisi?Ngano ishakua tatizo huko Middle East na North Africa kufuatia vita hii.
 
Soma tena ulichoandika then evaluate your self kama kweli unajua vzuri the deep source ya urusi kuivamia Ukraine....Unajua madhara ya USA kuivamia Iraq? Unajua madhara ya USA kuisapoti Israel vitendo vyake juu ya parestina?? Je wakati USA inafanya haya ulishakuja hapa kukemea kama Sasa unavyokemea urusi juu ya Ukraine?? Kasome vzuri juu ya Urusi na Ukraine usikurupuke ukadhani unajua kila kitu "Russia had no option than this happen now"
 
usitudangaye kijana sisi sio watoto kyiv imeshikwa vibaya rais wao analialia tuu.
Kushikwa pabaya sio tatizo, lkn jeshi Mrusi ataweza kuhimili vita hivi kwa miezi mitatu au zaidi ijayo. Uchumi umeanguka, silaha ambazo ndio zilikuwa zinamfanya awe Super power namb mbili duniani ndio hizo zinazidi kutumika kujilinda, askari wanakufa, wanajeruhiwa, wanatekwa nk. Wakati Mrusi akipanga namna ya kutumia silaha zaidi ili a win mapambano, Mmarekani na washirika wake wao wanatumia muda huo kuendelea kuunda silaha mpya, kukuza uchumi wao, na kujizatiti zaidi kwa ajili ya vita vya serious vinavyoweza kutokea huko mbele. Sio hivi vya mtoto na baba au vita ya paka na panya.
 
angalia kyiv inachofanywa huko acha kupepeta domo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…