LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Bottom line: Urusi imeivamia Ukraine na hakuna aliyefanya chochote kuizuia isiivamie.

Hata Marekani iliivamiaga Iraq kwa sababu za uongo na hakuna aliyefanya kitu.
Sasa inafaa hata kwenye vijitaifa vyetu tuheshimiane, kwenye haki kwa wote na demokrasia ya kweli. 🤔
 
Remember Hii sio 1945 Hitler no internet .Vita ni ushetani Sasa Hivi .Putin ashaanza ushetani ataendelea na Hitler alianza kuvamia one country to another walivyomstukia it was too late .Wasirudie mistake
Huyu Putin yuko sahihi kwenye hili acha kumfananisha na Hilter wa 1945. NATO na Marekani wana nia ovu kwenye hii dunia. Uingereza iko hatarini kuangamia kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, kiinchi kinakaribia kumezwa na bahari na kupigwa na vimbunga vizito. Kama Urusi na Uchina vikisambaratika wataanza vita ya kutafuta makoloni upya kwa sababu kuu mbili, kwanza kupata sehemu mpya ya kuhamia (kuhamishia watu wao na activities zao), pili kwenda kutunza misitu na kupanda misitu mikubwa ya kunyonya joto. Sasa hivi kikwazo kwao ni Russia na Uchina baasi.
 
Breaking: Nukuu ya Rais wa Ukraine!

Hali Ni tete kwa RAIS wa Ukraine aliyeanua kuonba Mazungumzo na RAIS Putin ambaye amegoma

Imebidi aongee na RAIS wa ufaransa aliyezungumza na Putin

"Russia will have to talk to us sooner or later about how to end hostilities and stop this invasion," he said.

"The sooner the conversation begins, the smaller Russia's losses will be."
 
Wewe jamaa umenichekesha sana..
Yaani mzuka umepanda yaani hasikii wala haambiwi yaani..mbele kwa mbele yaani
 
Breaking: Nukuu ya Rais wa Ukraine!

"Russia will have to talk to us sooner or later about how to end hostilities and stop this invasion," he said.

"The sooner the conversation begins, the smaller Russia's losses will be."
Mbona anaomba kwa mkwala namna hiyo?
 
Breaking: Nukuu ya Rais wa Ukraine!

"Russia will have to talk to us sooner or later about how to end hostilities and stop this invasion," he said.

"The sooner the conversation begins, the smaller Russia's losses will be."
Huyu Raisi wa Ukuraini jinga kabisa, Putini hakua na option nyingine zaidi ya kuvamia huyu mjinga utaleta je adui wangu kwenye mlango wangu?
 
We jamaa, uko sawa kichwani?? Mbona hukushangaa USA kushindwa AFIGHANSTAN??
 
Huyu lazima tumweke kizuizini maana watu tumeacha shughuli zetu na kuja kwake then anataka Po. You must pay and you will pay us,
 
mdogo wangu nyani na wewe umeingia mtego wa "maamuma"? unashabikia nchi huru kuvamiwa?
MAREKANI KWA MIAKA 300 ya uhuru imewahi kuiteka nchi na kuifanya sehemu yake? Iraq , Libya, somalia zimechukuliwa na kufanywa sehemu za USA?

URUSI wanavamia na kuteka nchi na kuzifanya sehemu zake, wewe upo hapo?

tatizo la Tz utapiamlo wa akili.
 
Ni kweli ila ni km 15 tubtoka Kyiv
 
Wewe jamaa umenichekesha sana..
Yaani mzuka umepanda yaani hasikii wala haambiwi yaani..mbele kwa mbele yaani
Kwanza manyimbo yenyewe yanayoimbwa na askari wa urusi ni hatari. Morali ipo juu sana na wakimuona kamera man wanamwita wapige picha taani wapo comfortable sana. Tanzania tuna jambo la kuiga hapa. Kuna kitengo kinaumiza na kufikilia mashambulio na kuna kikosi chenyewe kinaimba tu toka juzi hakifikilii wala kuwaza chenyewe kinasubilia Go ahead tu na ndio wanaolipua huko
 
Hahahaaa amechelewa.
 
Kwa hiyo kwako kuvamia, kuiangusha serikali iliyopo madarakani, kuharibu kila kitu ikiwemo amani, kwa sababu ya uongo, halafu baadaye unatimka na kuiacha vurugu uliyoianzisha, ni sawa kwa sababu hukuifanya hiyo sehemu iwe sehemu ya nchi yako?

Watu wawili wote mnaweza mkawa na makosa lakini makosa yenu yasifanane.

Wewe hapo ulipo unaona Marekani ilikuwa sahihi kabisa?
 
Ukraine yavunja Daraja kuchelewesha Askari wa Urusi kuteka mji mkuu, wakati huo huo Marekani inajiandaa kupeleka msaada wa kijeshi wa 600 million USD.

Pia Kuna Taarifa za Urusi imepoteza Umiliki wa Uwanja wa ndege waliouteka, na vikosi vya Urusi kushindwa mpakani mwa Beralus.

Why Ukraine hata wakipigwa wanatoa taarifa ila Urusi anaficha
 
Tatizo ni kwamba watu walifurahia ISRAEL kushambulia PALESTINA ambapo waliliweka kwenye mlengo wa kidini.
 
Tafadhali naomba ufunguke vizuri. Umeongea vitu vizito sana vya kiroho na hivyo inabidi uviweke wazi ili tuweze kuelewa na hiyo ndiyo itakuwa faida kwako na kwetu pia. Tafadhali naomba utufanunulie vizuri maelezo yako haya, yako kitaalamu mno kiroho!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…