LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
 
Vita sio mchezo kaka Russia nae ana isoma nambaView attachment 2130502
Ndugu yangu, mimi nime subscribe na kufollow account tofauti tofauti kuhusu hii vita na bahati nzuri zote za Ukraine.

Anachokifanya kwa sasa Ukraine kwa % kubwa ni ambush! Wanapofanikiwa ndiyo hizo taarifa unazoziona. Na hayo mambo ni machache na ndiyo maana taarifa za hayo matukio ni chache na nyingi zinajirudia hata ukizitafuta Internet. Ni suala la propaganda na kwenye vita ni suala zuri.

Nimebahatika kuona video za Urusi mashambulizi wanayoyafanya Ukraine na matokeo yake inasikitisha sana. Wanajeshi wa Ukraine wameungua ungua. Wengine wamepigwa risasi wamekufa. Magari yao na vifaru vyao vimelipuliwa na maiti zao zinatolewa.
 
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky usiku huu amesema kwamba kwa mujibu wa takwimu za awali Wanajeshi wa Ukraine wasiopungua 137 wameuawa tangu uvamizi wa Urusi uanze ndani ya Nchi hiyo huku Wanajeshi 316 wamejeruhiwa.

My opinion:
Vita ni jambo baya sana. Sisi tunashabikia humu ila hapa kuna watu wanazika baba zao, kaka zao, wajomba n.k sababu tu kuna mtu mmoja aitwaye mwanasiasa hatakiwi kupingwa.
 

Hayo ndio mambo NATO inafanya wanaenda kufanya military training Baltic Sea kila siku kwa madai ya Ukraine Waters.

Russia amewavumilia sana uchokozi wao naona kaona isiwe shida ngoja aimudu Ukraine kwanza. West ni wazuri kwenye propaganda ila deep down wao ndio wachokozi.
 
Kwa kinachoendelea si nafuu kabisa kwa wanadamu wenye kuvuta hewa na kinachotakiwa inferior (Ukraine) ajishushe tu kwa Russia(superior) hii itapunguza maafa kwa watu wasio na hatia kabisa Tena wa mataifa mengine. Na hili TANZANIA tujifunze kwa majibu waliopewa majirani kutaka kutia mguu
 
Chochote kinachotokea hapa duniani huwa kina chanzo. Ukiangalia chanzo cha mgogoro uliopo kati ya Urusi na Ukrane, ni mmojawapo kuwa tayari kujiunga na NATO, ambapo kwa hali ya usalama kwa Urusi, ungekuwa ni mdogo.

Ni sawa na ujenge nyumba kubwa nzuri , uoe mwanamke mrembo aliyemaliza chuo mwaka jana na ukaishi naye; baada ya mwezi mmoja , ukasikia jirani yako mnaeshea naye ukuta, anataka apangishe nyumba yake kwa mpenzi wa zamani wa mkeo aliyesoma naye chuo.

Hapo lazima, uwe mkali kwa sababu itakuwa ni hatari kwa ndoa yako. Hicho ndio chanzo cha mgogoro unaoendelea kwa sasa.
 
Binafsi sipendi vita, na sipendi kuona mtu au nchi ikichukua uhuru wa nchi nyingine.

LAKINI naweza kusema kwamba Rais Putin yuko sahihi kulinda maslahi ya nchi yake. Kumbuka Ukraine ni zao la USSR, kwa namna moja hii ni sawa na territory au state ndani ya USSR...Ingawa hii haifanyi kazi au sio hoja kwa sasa.

Hoja ni kwamba NATO inatumiwa na US kwa nia ya kutaka kuisambaratisha Russia. Putin kuzuia uwepo silaha za NATO ndani ya Ukraine ni sawa na US ilipopiga Cuba sanctions kwa kuruhusu Russia kuweka silaha zake pale. Russia hakuwa na nguvu tena Cuba, na uchumi wa Cuba ukambaratika. Juzi juzi Russia imetaka kusaidia Venezuela, US kapiga pin kufanya mpango wa kumuondoa kiongozi madaraka. Huwezi temper na US security na interests akuache salama, sasa sijui kwa yeye ni ngumu kukubali wengine kulinda interests zao.

Ni kweli US hajapora ardhi, ila madhila alioyoacha Iraq, Afghanistan, Iran ni makubwa sana...yaan bora angechukua nchi maana wananchi wasingekuwa wanahaha na ugumu wa maisha.

USA ina sifa kubwa ya kutetea demokrasia na haki na kutoa misaada yenye kugusa maisha ya watu maskini na wahitaji (binafsi dola ya mmarekani imenisaidia binafsi), ILA ktk agenda ya democracy kuna linaumiza baadhi ya watu.
 
futa hii,
uislam hauna uhusiano na lolote huko...
wakristu sijafuatilia kama wametoa tamko
 
Tatizo ni kwamba watu walifurahia ISRAEL kushambulia PALESTINA ambapo waliliweka kwenye mlengo wa kidini.
Si kwamba tunataka Ukraine ipigwe na Urusi.Tunachopendelea Ulaya na Marekani washindwe ndani ya Ardhi ya Ukraine.
 
Uvamizi wa Russia ni wa kistaarabu kiaina. Russia hajalenga civilians kabisa, hata hiyo kufa kwa civilians 130 ni ajali.

Russia inataka military infrastructure hasa hii misaada ya juzi.

Ni ngumu hata NATO na US kumshambulia, wataishia kwenye sanctions tu.
 
Sasa huyo poland anasubiri nini kuingia vitani? Na msimsingizie poland, USA na wenzie waingie waone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…