Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

That's why we keep saying that every sane person from the third world, particularly from Africa, should support what Putin is doing.
 
Ukweli mgumu kuhusu mzozo wa Urusi na Ukreni hatimaye unawazukia nchi za Magharibi

Wachunguzi Wamarekani hatimaye wanazinduka kwenye ^fikra ya kimazingara^ kuhusu kushindwa kwa Mosko.

Na Tarik Cyril Amar, mwanahistoria kutoka Ujerumani afanyaye kazi katika Chuo Kikuu cha Koç, Istanbul, akijihusisha na Urusi, Ukreni, na Ulaya Mashariki, historia ya Vita II vya Dunia, Vita Baridi vya kitamaduni, na siasa za kumbukumbu.

Mnamo Novemba 16, Jarida la Wall Street, moja ya vyombo vya habari vyenye hadhi na ushawishi mkubwa zaidi Marekani, lilichapisha makala chini ya kichwa cha habari ^Ni Wakati wa Kukomesha Mawazo ya Kimazingara Kuhusu Kuishindwa kwa Urusi.^

Waandishi husika, Eugene Rumer na Andrew S. Weiss, ni wawakilishi wenye ushawishi wa usalama wa taifa la Marekani na ikama ya mahusiano ya kimataifa.

Baada ya ajira katika utumishi wa serikali, Rumer sasa anaongoza programu ya Urusi na Eurasia katika Asasi ya Carnegie kwa ajili ya Amani ya Kimataifa; Weiss ni makamu rais wa Carnegie kwa ajili ya tafiti mbalimbali. Haya ni maandishi muhimu, na ujumbe na muda wake wa kuchapishwa vina maana.

Ujumbe husika ni rahisi: ^Putin^ (ambapo wanamaanisha Urusi) ^amehimili juhudi bora za Magharibi^ kurudisha nyuma operesheni ya kijeshi dhidi ya Ukreni; mfumo wa kisiasa wa Mosko umethibitika kuwa madhubuti na hata kuwa na imara zaidi; na ^Marekani pamoja na washirika wake^ lazima sasa wageukie mkakati wa ^uzingaji.^

Muda ambapo tukio husika linatokea ni changamani zaidi. Ni wazi, vita vya sasa vya Israeli dhidi ya Gaza—vijulikanavyo kama ^msukosuko katika Mashariki ya Kati^—ni moja ya mambo matatu muhimu.

Mengine mawili ni uchaguzi wa urais unaokaribia nchini Marekani, na kwa kweli, kushindwa kwa mashambulizi-pinzani ya Ukreni katika msimu wa hari, ambayo kwa sasa yamekiriwa hata katika vinahabari kindaki kama vile British Daily Telegraph.

Pamoja na hilo, ushawishi wa Marekani juu ya idadi kubwa ya watu wasio wa Magharibi unaenelea kupungua. China, hususan, inafanikiwa kupinga shinikizo la Washington.

Ndani ya nchi, serikali ya Rais Joe Biden inakabiliwa na pepo mbisho na kali kutoka kwenye upinzani rasmi wa Republican na vuguvugu linalokua katika mitaa ya Marekani, ambapo hali ya kina na pana ya kutoridhika na siasa na uchumi sasa inachanganyika na mfutuko usio kifani wa maandamano dhidi ya ushiriki wa Marekani katika vita vya mauaji ya kimbari ya Israeli kwa Wapalestina.

Kura za maoni Marekani hazina utata. Mnano Septemba, hata kabla ya mzozo wa Mashariki ya Kati, Kituo cha Utafiti cha Pew kilibaini kwamba ^mitazamo ya Wamarekani kuhusu siasa na maafisa waliochaguliwa,^ kwa namna isiyo ya kawaida na ^isiyopungua, sasa ni hasi, ikiwa na tumaini dogo la kuboreka mbeleni.^

Kufikia sasa, Wamarekani wengi pia wanapingana na utawala wa Joe Biden—na karibu taasisi zote za kisiasa za pande mbili—kwa kutaka kusitishwe mapigano huko Gaza, wakati idadi ya wale wanaounga mkono Israeli inapungua haraka na kwa kiasi kikubwa.

Kutokana na hali hii, makala haya ya Jarida la Wall Street hutumika bayana kama wito madhubuti wa kubana matumizi.

Lengo la ishara hii ya kurudi nyuma ni vita vya uwakala nchini Ukraine, yaani, mkakati mmoja mkali zaidi, hatari zaidi, na ulioshindwa zaidi wa sera ya kigeni ya Marekani katika miaka miwili iliyopita (ikiwa tutahesabu kuanzia wakati Washington ilipoamua kizembe kuzorotesha onyo la wazi la Mosko na awani yake ya haraka ya kutafuta mbinu ya majadiliano kwenye njia-panda mwishoni mwa 2021).

Hadi hapa, tukio zima hujieleza hasa. Lakini haishangazi. Kwa sababu mbili: kugeuka kutoka Ukreni tayari ni suala la zamani ambalo kimsingi si habari tena.

Hata vyombo vikuu vya habari viliona kuibuka kwa hali mbaya, pengine ya hatima, ya uchovu wa Ukreni kabla ya kuzuka kwa vita mpya katika Mashariki ya Kati.

Pili, mawazo yenye mashaka ambayo sasa yamepewa kipaumbele katika Jarida la Wall Street Journal kama sababu za kusitisha uwekezaji wake wa vita vya uwakala nchini Ukreni hakika ni ile kofia ya zamani. Kwa kweli, swali la kuvutia zaidi ambalo makala haya—bila kukusudia—huibua ni nini kilichofanya mchukue muda mrefu hivyo?

Itakuwa suala la kuchosha kuainisha kila hoja iliyoibuliwa sasa katika Jarida la Wall Street. Lakini kwa vile zote zina utangamani kwamba zilikuwa zimetabiriwa au zilikuwa zikitabirika kabisa, dondoo chache zitatosha.

Tunagundua, kwa mfano, kwamba majaribio ya Magharibi kuitenga Urusi yameshindwa. Hata hivyo ni kwa namna gani hilo lilikuwa gumu tanabihi kwamba Ulimwengu wa Kusini hauna sababu ya kuifuata Magharibi isipokuwa hofu, na hofu hiyo inapungua?

Na hivi haikuwezekana kujua mapema kwamba China ingejibu ^Hapana, asante sana,^ pale Marekani na EU zilipofanya mambo mawili kwa wakati mmoja: zilipoihimiza kuachana na Urusi, ambapo ingemaanisha kuachana na ubia muhimu sana wa Beijing, na kuashiria kwamba China nayo ingefuatia kukatwa vipande-vipande?

China, kimsingi, awali ilionesha dalili ndogo katika uelekeo wa kujitenga na Urusi, lakini misingi ya kimkakati ya hali hiyo iliamua mwenendo wake halisi na umekuwa wazi kwa sasa. Matokeo haya yalitabiriwa, siyo na kila mtaalamu lakini na wa kutosha miongoni mwao kiasi cha kulipa umuhimu jambo hili.

Pia tunakumbushwa kwamba hivi ni vita vya msuguano, yaani ambavyo kwa asili yake vinaipendelea Urusi. Hata kwenye CNN, tulisikia hivyo mapema Aprili 2022, na jarida la kivita la Atlanticist Economist lilikiri hilo kiutata (likitumia tafsida ya ^vita vya uhimilivu^) mnamo Septemba.

Kila vita ni suala la utendaji shindani wa kijeshi. Lakini katika vita vya msuguano, mambo matatu ya msingi ni muhimu zaidi: ukubwa, uwezo wa uzalishaji na wa kiteknolojia, na uhimali wa uchumi; uthabiti wa mfumo wa kisiasa, pamoja na umaarufu wake halisani na uhalali wa maahari wake; na, bila shaka, demografia.

Jarida la Wall Street Journal linabaini kwamba uchumi wa Urusi ^umekumbwa na pigo kali lakini haujaparaganyika^ (likitweza hasa mafanikio yake, lakini hebu tusibishanie mambo duni) na kwamba mfumo wake wa kisiasa unategemea uungwaji mkono ^imara^ na maahari ambao hawajawahi kamwe kuasi wala kutoroka.

Katika nchi za Magharibi angalau, hii ilikuwa ngumu kutabiri. Siyo sababu ya Urusi kuwa ngumu sana kuing’amua, bali kwa sababu ya ubaguzi wa Magharibi na fikra muwala, au, kwa kusema wazi, matarajio potofu.

Hata kabla ya vita vya Ukreni Februari 2022, siasa za Magharibi, vyombo vya habari, magalacha, na hata wanataaluma wametunuku tathmini hafifu zisizo halisi za uchumi wa Urusi na uthabiti wa kisiasa.

Fikiria, kama sampuli mojawapo, mitilifiko ya Magharibi kufuatia uasi wa Wagner mnamo Juni. Wachache miongoni mwao walitabiri anguko la karibuni la Urusi na kutokea machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe au, angalau, tukio kubwa na la kudumu la kudhoofika kwa ndani na kimataifa kwa Urusi. Hata hivyo hakuna hata mojawapo ambalo limetimia.

Umuhimu wa uchanganuzi na utabiri huu wa kina, takriban wenye uelekeo wa kushindwa kabisa hutokana na jinsi ulivyokuwa wa aina yake, ukiakisi utamaduni tawala wa uzembe wa kisiasa udhoofishao fikra za Magharibi kuhusu Urusi. Uzembe unaoshangaza zaidi ambao hasa wapinzani wa Mosko hawawezi kuutenda bila kujiumiza vibaya.

Kwa vile kujidhuru wenyewe ndio matokeo yake makuu. Ni kweli kwamba Urusi haina budi kubeba baadhi ya gharama za maradhi ya Magharibi ya kutoona mbali.

Ni wazi, Mosko pia ingekuwa heri zaidi iwapo ingeweza kufanya kazi na washirika wenye busara, kama ni wenye ushindani, badala ya wapinzani wenye uhasama wa akili ambao daima huitweza Urusi na kujikweza wenyewe.

Licha ya hayo, nchi za Magharibi zinateseka hata zaidi kutokana na mtindo wake wa makosa ya kujirudia.

Gharama za vita vya uwakala nchini Ukreni huonyesha ukweli huu, na siyo tu katika mantiki ya silaha na pesa, bali kuhusu hadhi ya kisiasa pia.

Kuhusu gharama zinazoweza kukadirika, Bunge la Marekani, kwa mfano, limeidhinisha msaada wenye thamani ya dola bilioni 113 kwa ajili ya Ukreni tangu Februari 2022.

Hivi sasa, ombi la kutaka hata zaidi linageuka kuwa maumivu makubwa ya ndani kwa utawala wa Biden, na huenda kabisa, kushindwa kwake. EU imemwaga takriban €85 bilioni.

Kwa kweli, siyo kwamba fedha hizi zote zimetwaliwa, na kiasi chake kikubwa kimekuwa hasa kikichochea ufisadi nchini Ukreni au kuwahudumia wafadhili na hususan viwanda vyao vya kutengeneza silaha, kama ambavyo wanasiasa Wamarekani wameeleza mara kwa mara kwa dhihaka za majivuno.

Lakini picha nzima inasalia kuwa ile ya matumizi makubwa ya fedha kwenye kamari iliyopotea. Ongeza hasara ya kujitakia ambayo uchumi wa Umoja wa Ulaya hususan umepata kutokana na sera yao ya vikwazo dufu, ndipo picha hiyo huonekana kuwa mbaya zaidi.

Ongeza, zaidi ya hayo, kiasi ambacho Magharibi italazimika kutumia iwapo inataka kweli kufadhili ujenzi mpya wa Ukreni, na ndipo matarajio hugeuka kuwa janga kuu. Kila la heri, EU, na hiyo mipango ya uanachama.

Aidha, vitu visivyoonekana ni muhimu pia. Ni wazi, ^kuipoteza^ Ukreni (ambayo Magharibi haingepaswa kujaribu ^kuimiliki^ hapo awali) kutafichua mno udhaifu wa kambi hiyo kuliko kushindwa katika, kwa mfano, Iraki, Libya, Siria, au Afghanistani. Kwa sababu mbili. Kwanza, tofauti na nchi hizi, Urusi ni himaya kubwa; hilo humaanisha iko katika nafasi ya kujinufaisha na mtanziko wa Magharibi.

Mosko, kwa kuiweka kwa namna tofauti, ni kubwa vya kutosha kukabiliana kijiografia.

Iwapo au lini hasa itafanya hivyo, na ni sura gani ambayo ^mfyatuko^ mpya wa sitiari ya ^ukanda wa raba^ ya Rais Vladimir Putin wa Urusi utachukua wakati huu, ingali ikitizamiwa. Jambo dhahiri ni kwamba malipo kama hayo ni uwezekano halisi.

Pili, nchi za Magharibi zimeazimu kuliko wakati wowote uliopita, kwa rasilimali na maneno, inapojaribu kutumia Ukreni kuipunguza Urusi. Hivyo, kushindwa kufanya hilo hufichua ukomo wa Magharibi kuliko wakati wowote uliopita.

Rumer na Weiss si malimbukeni. Hawawezi kusema hilo—na labda hawawezi hata kulifikiria kabisa—lakini ndani kabisa ya mioyo yao wanajua kwamba kufungasha hali hii ya kushindwa na kuifanya ionekane ni badiliko tu la kimkakati kuwa ^uzingaji^ haitampumbaza yeyote asiyetaka kudanganywa.

Ni vyema hatimaye kuona baadhi ya habari ngumu za kweli zikionekana wazi katika mijadala mikuu ya Magharibi. Lakini haitoshi.

Kwa ajili ya jambo moja, nchi za Magharibi zinapaswa kujiuliza maswali machungu kwa nini zimedumu kushupalia upande mmoja muda mrefu kiasi hicho.

Vinginevyo, mtindo uleule utarudiwa katika kuanzisha na kuendesha vita vinavyofuata, kwa mfano, dhidi ya China au Irani.

Pili, kuhamia zoezi la ^uzingaji^ hakutarekebisha uharibifu bali kutaongeza tu.

Kile ambacho nchi za Magharibi zinahitaji hasa ni kufikiria upya kabisa, siyo tu kuhusu mbinu zake bali malengo yake.
 
Kwenye Vita ikiwa mnaubonda mwingi...... automatically mnakuwa na morali ( motivated) kupigana Kwa nguvu .......but vice versa is true ikiwa mmezidiwa basi hakuna atakyetaka kwenda front

Nadhani that's real happening ni kiev right now....watu hawana hamu na red army
 
Thank Member
 
View attachment 2826589

Russia is now mass producing helicopter drones. These mini helicopters can fire rockets and drop bombs
How have they done this with limited scrap washing machines and few gardening tools?
Zitatunguliwa tu....

Ukraine wanajua namna ya kuzidanganya AD za Urusi.


T14 Armata
 
Kwani kuna ulazima ucoment hujioni umebaki peke
Mwacheni kp kipanya44 ajiliwaze kwa mia nane, mia sita, mia tisa wake aliowachinja, bila hivyo anaweza kurukwa akili.

Kwenye SMO ya Urusi, amebaki yeye na Zelensky tu kwenye Team Ukraine.

Hata EU na Marekani wenyewe hawawatambui tena. Sorry for them!
 
Mambo mengine wala sio ya kushabikia kwa kweli, zelensky anapelekea vijana wa Ukraine kufa kama sio binadamu vile Lisa ni hataki kua nyutro,yeye anataka kua NATO hasimu wa Urusi.yaani kachagua kumkaribisha adui wa jirani nyumbani kwake.
Miili 200 imeachwa na wanajeshi wenzao wa Ukraine wakati wakikimbia mapigano.
Onaumiza sana.
Hii sio nzuri aisee.


MILITARY OPERATION IN UKRAINE
29 NOV, 10:37

Ukraine’s army abandons about 200 dead soldiers in hasty retreat near Donetsk, says DPR​

Russian forces are now evacuating the bodies of dead Ukrainian soldiers, Yan Gagin noted

The Ukrainian military abandoned about 200 dead soldiers in its hasty retreat from its positions near Donetsk, Yan Gagin, adviser to the head of the Donetsk People’s Republic (DPR), told TASS on Wednesday.
"The abandoned Ukrainian positions near Donetsk are strewn with a huge number of the bodies of Ukrainian soldiers who were deserted. In fleeing the area, the enemy did not even try to evacuate them. We have counted about two hundred [of dead Ukrainian soldiers] so far," the adviser said.
Russian forces are now evacuating the bodies of dead Ukrainian soldiers, he added.
The adviser to the DPR head told TASS on November 10 that the number of Ukrainian soldiers entrenched in first defensive line positions near Donetsk had dwindled at least threefold due to their fleeing.
 
Nadhani Picha kamili unaiona hata humu jukwaani,
Wale wafia NATO wote wametoweka.
Wanakujaga TU kama kifaru ama ndegevita ya Urusi ikipigwa.
 
Dah,unajua Urusi ni wababe wa NATO?
Ama Kwa hakika Dunia imejua yaliyokua yamejificha.
Ama Dunia imesimuliwa the untold stories.
Medvedev kwa dharau kubwa anwaambia safari ya meli ya vita itakayoanza Jan 5 itakua ambayo itazungukia maeneo ya NATO ni zawadi ya krismass Kwa NATO,na katoa vitisho kibao kwa wababe wa wanyonge (NATO).

Medvedev sees Russian frigate’s trip as `New Year gift' to NATO​

He said the frigate carrying Tsirkon hypersonic missiles which began its trip to NATO’s shores yesterday was "a major New Year gift

The Russian frigate Admiral Gorshkov’s entering combat duty on Wednesday should bring anyone who will dare pose a direct threat to Russia to their senses, the Deputy Chairman of Russia’s Security Council, Dmitry Medvedev, warned on Thursday.
Medvedev said the frigate carrying Tsirkon hypersonic missiles which began its trip to NATO’s shores yesterday was "a major New Year gift." "Rejoice! [It] will bring anyone posing a direct threat to Russia or our allies to their senses," the politician wrote on Telegram on Thursday.
"We will use force against you, since you refuse to understand what we have been saying," Medvedev warned, adding that Russia will produce more cutting-edge weapons.

Kudadadeki
 

Hungary will never send weapons to Ukraine, top diplomat says​

Budapest will never send weapons to Ukraine because weapons supplies only prolong the conflict, Hungarian Foreign Minister Peter Szijjarto said.
"What we have never done and will never do is weapons deliveries because we do believe that instead of weapons, peace should be brought to this region. The more weapons are delivered the longer the war will take; the longer the war takes, the more people will die," he pointed out in an interview with CNBC.
 
The most sensible comment ever. These are the kind of leaders such as should receive our unwavering support.
 
Walipo anzisha Mashambulizi yao Walisema Vuta vilianzia Cremea Na vitaishia Cremea
Sasa Bakhmut Ndio inazidi Kutanuka Kuwa Chini ya Urusi
Sehemu zilizokuwa Bado Hazijakombolewa ndio Zinazidi Kukombolewa

Khromovo is now under Ru control, this area was never captured by Ru in the battle of Bakhmut which ended in May of this year.
 
Wasipoangalia Taifa la Urusi litawadhalilisha hao NATO.
Pia Zelensiky asipofikiri vizuri atawaua Vijana wengi wa Taifa lake sababu Mtu anayepambana nae akipigana na Marekani direct HAKUNA Mshindi.
 
Mkuu unajionaje baada ya comment hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…