Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kitendo Cha USA na UK kushilikiana na Ukraine kushambulia Makazi Raia mpakani mwa Urusi, badala ya kushambulia kambi za Kijeshi ama ghara za silaha ni aibu kubwa.
Wameonyesha vile walivyo kuwa ni mashetani.
Juzi walishababisha tena Vifo vya Wa Ukraine 39 baada ya Air defence kukosa Target na kulipua nyumba za Wananchi wao.
Unawezaje weka Siraha Kama hizo uraiani? Ukijua zinaweza lipuliwa na kuua ama kukosea shabaha na kuua Wananchi wako mwenyewe.
Heshima ya Amani tuliyowapa UK na USA Sasa haipo kwa vitendo vyao vya uhasama kwa Mataifa ya Palestine na UKRAINE. Vita hivi wamesababisha wao kwa manufaa yao. NIMEWAZARAU.
 
Mzee wa data kutoka Kyiv Independent, vipi leo mumeua mimashine tu bila watu?!!
 
Hii ni sababu nyingine ya kwa nini ni vigumu kwa Ukraine kuweza kushinda, kushinda vita kwa kutegemea silaha za msaada ni changamoto labda kama huo msaada ungekua unakuja vile ambavyo wewe unataka. Mf Ukraine akitaka 300 F-16 basi zije kwa wakati, akitaka 500 tanks zije kwa wakati, na ni kitu ambacho ni ngumu kuwa implemented.

viwanda vingi vya silaha vilibomolewa na makombora ya urusi mwanzoni sana kwenye mgogoro huo hivyo kupelekea kutokua na viwanda vingi vya kuzalisha silaha, inabidi sasa kutegemea misaada ya nchi washirika.

Ripoti nyingi zimeonyesha uhaba wa silaha kwa nchi za west hivyo inapelekea sapoti yao kwa Ukraine kuwa ndogo.

Ila kwa upande mwingine, sapoti ya west inaonekana ni ndogo kwa sababu ya opponent ambaye Ukraine anapambana nae. Binafsi naamini msaada wa silaha wa zaidi ya $40 Bil sio mdogo, ni msaada mkubwa sana wa kijeshi.

kuna ripoti moja wamemcite Estonian defence official akawa anasema Russia wanatengeneza ammunitions 7 times zaidi ya western.



Sasa ili kuleta balance ya vita ilibidi nchi za west ziwe zina supply ammunitions kwa speed hiyo hiyo ambayo Russia anatengeneza.

Na kutokana na "kiwango kidogo" cha silaha ambazo Ukraine wanapata, na ili kurudisha mashambulizi kwa Russia, inapelekea wanazi "overuse" silaha na zinapelekea kushindwa kufanya kazi sawasawa. Lakini pia NYT waliandika kipindi flani kwamba ile speed ya western kusupply silaha kwa Ukraine, walikua wanapeleka silaha ambazo ni "unusable"

Mfano;
-Faults zilianza kuonekana kwenye Italian FH70, Krabs, Caesar and German PzH 2000 howitzers.

-Italian FH70 ilikumbwa na changamoto ya kupungua kwa Nitrogen pressure kwenye gun balancing mechanism.

-PzH 2000 za wajerumani zilikumbwa na issues za overheating kwenye control unit monitors (Overuse?? Walikua hawaruhusu enough cooling time??)

-waukraine pia waligundua matatizo kwenye PzH 2000 za wajerumani hapa ishu ikaja kuwa kwenye kufeli kwa obturator rings na charging system za PzH 2000 howtizers. Pia kulikua na error messages zinatokea baada ya intense shelling (Overuse??)

-M777 za waingereza zilikua na changamoto ya kuretract the barrel baada ya frequent firing (Overuse??)

-Krab howitzer za wapoland pia zilikua zinapatwa na changamoto ya kuvunjika kwa shaft na wedge bolts baada ya heavy firing (Overuse??)

-Caesar howitzer za wafaransa zilikua na changamoto ya kufeli kwa guidance blocks na aiming program ambazo zilikua zinacalculate shots kimakosa, zikapelekea kwa shots kuwa "undershot"

Inawezekana sababu ikawa ni overuse bila timely services au ikawa ni ile mizigo waliyoletewa haraka haraka ambayo haikua stable kuingia kwenye battlefields.

Ukraine angekua bora zaidi kivita ila aliingizwa "mkenge" alafu akajaa. Ukraine alikua na vitu kama Tu-160 strategic bombers, strategic Tu-95 bombers, na Kh-55 air-launched cruise missiles na vingine vingi....

Sasa nini kilitokea? Mengi yalitokea. Mfano wa yaliyotokea;

Under the Cooperative Threat Reduction (CTR) program, the United States has assisted Ukraine with dismantling remaining heavy bombers, strategic air-launched cruise missiles, and ICBMs and associated silos and launch-control centers.



 
Hii ni kama kusema unataka kwenda Rwanda ila unapita Uganda the. Rwanda[emoji23][emoji23]
 
Da huu sio uchambuzi,Bali ni kutupa maarifa.
Kusema kweli umetupa maarifa yavhali ya juu mno.
 
Khinzal ni moto mwingine [emoji23][emoji23]
Jamaa kawatia dole kweli kweli; kitu ikipota Hadi jirani na kambi za US na NATO alafu hiyo ikaenda kufanya yake

The incident with a russian cruise missile entering Polish airspace is more than just a "demonstration of power" on the side of russia because it happened near military bases used by the USA and Bundeswehr

 
Halafu utamu wa hii habari wameielezea Poland wenyewe badala ya mhusika mwenyewe (Russia). Jamaa kanyuti tu anawasikilizia wanavyotoa maelezo.
 
Halafu utamu wa hii habari wameielezea Poland wenyewe badala ya mhusika mwenyewe (Russia). Jamaa kanyuti tu anawasikilizia wanavyotoa maelezo.
Kuna mchambuzi Moja kasema hii itakuwa Russia aliamua kutest air defense za NATO aone kama ziko viti.

Hii inathibitisha Ile kauli ya Rusia kwamba anaweza twanga Europe ndani ya masaa machache mno
 
Uzi umepoa sana asee ... Yaan cjaingia kwenye hii thread na almost 2 weeks but leo naona page chache kuliko expectations zangu
Ndugu yangu usiombee Uzi huu kuchangamka,maana ukiona Uzi huu unachangamka ujue Kuna watu wanakufa.
Mimi katika mzozo huu naiunga mkono Urusi,lakini naumia sana mzozo huu kutatuliwa Kwa njia ya vita.
Ukweli ningefurahi sana kama Ukraine Ingekua nyutro kama Urusi ilivyopendekeza.
Lakini west wamemtia kiburi nae akamkubali kuingia vitani na Urusi.
Kwa hiyo ukiona Uzi umechangamka ujue Kuna binadamu wenzako wanakufa,kupoteza viungo na Mali zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…