Lakini ukipelekwa USA ukaishi sidhani kama utataka kurudi Tena mavumbini huku bongo😀😀😂
[/QUO
Hapana Mkuu,nafikiri utakua anachanganya mambo.
Iko hivi,tunaposema Marekani ni shetani,hatumaaanishi maisha au raia wa USA ni mashetani.
Hapa hua tunalenga baadhi ya policy.
Kwa mafano katika hoja yangu na wengi humu,tunalenga sehemu Fulani ya Foreign policy ya USA ambayo ni ya kionevu kwa kweli.
Kwa mfano kama unavyoona Leo USA walishangilia ICC kuhukumu Putin akamatwe,lkn hao hao USA wanapinga Netanyahu asikamatwe na ICC.
Mafno USA wanapeleka Kila aina ya silaha east europe.wana nukes turkey,wanataka kupeleka nuke UK,wanasiasa Germany,Wana silaha Korea kusini,kn hawataki Urusi apeleke silaha Amerika ya kusini au latin Amerika kwa marafiki zakeWanapeleka silaha Taiwan lakini hawataki china apeleke silaha sehemu nyingine.
Wanatangaza Demokrasia Dunia lkn hawataki nchi zijiamulie mambo Yao,mfano nchi nyingi hazitaki mambo ya ushoga lkni USA wanazitishia kuzinyima misaada n hi hizo kama zisipoweka kwenye katiba zao mambo ya ushoga.
Ishu ya NATO.
Wanazishawishi nchi jirani na Urusi Ijiunge na NATO ili kuipiga Urusi baadae,lakini Urusi ikizishawishi nchi nyingine ziungane nayo nchi hizo zinzowekewa vikwazo.
Marekani wanakili wenyewe kua walihusika na mauaji ya maraisi kadhaa wa Afrika na wengine kuwapindua,pamoja Kuua watu mashuhuri wasiokubaliana nao,baadhi Yao ni kama Lumumba,Ghadafi, Bob Marley n.k
Mambo ya kishetani Kwa USA ni mengi mno.
Raia wa Marekani sio mashetani na hata maisha ya Marekani ni mazuri mno,yaani siasa za ndani za USA ni nzuri mno.
Sasa kama wamarekani wanzitesa nchi nyingine tuache kusema ?
Tuache kusema kwa sababu Marekani ni kizuri?
Je raia wa Marekani wanaoipinga serikali Yao kwa maandamano na mambango yanayoisema kua ni serikali ya kishetani nao wafukuzwe USA.
Wapo raia wengi wa USA na hata European wanaandamana Kila siku kuupinga NATO na kutaka ivunjike na kuitia ni NATO ni mashetani nao wafukuzwe ulaya na Marekani?
Nakumbuka wakati wa Bush niliona kwenye CNN raia wa USA wakiandamana na mabango yaliyosomeka "Bush the killing machine"
Tusiende mbali,Leo hii Kuna wanafunzi Kwa maelfu pamoja na watu wa kawaida wanaandamana huko USA na Europe Wana,iponga serikali zao kwa uonevu wao dhidi ya wapalestina ,je wanafunzi na raia hao wafukuzwe nchini kwao?
Ndugu yangu Marekani kama nchi na raia wake hawana taaabu kabisa,kwanza ni watu wema na wapenda wageni,nchi ya Marekani ni nchi nzuri na ya kupendeza kabisa,maisha ni mazuri kwa wenyeji na wageni,Sasa je kwa upendo wao huo na uzuri wao huo tuache kuikosoa serikali ya USA kwa mabaya
wanayozitendea nchi na watu wengine?