" Urusi anapigana peke yake na collective west na bado anawamudu"
Alisikika mywagongo Mmoja kutoka gongolamboto!
View attachment 3128639
Dah!
Aisee nyie Pro UkraiNATO safari hii mnapitia kipindi kigumu sana katika maisha yenu.
Mlikua mnaamini NATO na west ni Kila kitu,lkn mmekuta Urusi haitishwi na west NATO hata kidogo.
Hivi wewe Kwa akili ya kawaida TU unasema Leo hii umeposti hicho kitaarifa chako tokea ijumaa ya tarehe 18 -10-2024 kua eti Korea kaskazini inaisadia Urusi.
Hivi tufanye habari hii ni ya ukweli ingawa imewekwa kipropaganda.
Hebu ona hoja Yako ilivyokua haian mashiko.
Urusi iliivamia Ukraine tarehe 24 -2-2022,imepita miaka miwili karibu iwe mitatu Sasa,Leo hii tarehe 18-10-2024 ndio unakuja unaleta kitaarifa chako kua Urusi inasaidiwa na Korea kaskazini'.
Kwenye hicho kihabari chako wameandika Korea kaskazini "imeamua" kupeleka wanajeshi kuisaidia Urusi.
Sasa nakuuliza Hawa wanajeshi wa Korea kaskazini Kwa miaka karibu mitatu walikua wapi kuisaidia Urusi?
Je unaweza kufananisha sentensi kua Korea kaskazini imeamua kupeleka wanajeshi wake Leo tarehe 18-10-2024 na msaada walioutoa NATO na west wote walipoanza kuisaidia Ukraine kabla ya vita na kipindi chote tokea vita imeanza?
Maana USA UK German walianza kufundisha wanajeshi wa Ukraine kabla ya vita na wakaanza kuisaidia silaha fedha mbinu,taarifa na mafunzo nchi ya Ukraine mara tu vita ilipoanza.
Je huoni kama Urusi ndio nchi inayostahili heshima yake?
Maana nchi moja inapigana na nchi inayosaidiwa na nchi 59.
Na ndani ya nchi hizo 59 Kuna NATO,sio NATO tu bali na nchi nyingine za west.
Sina uhakiaka na hiyo habari Yako.
Lakini haya kama itakua ya kweli je Urusi Hana haki ya kusaidiwa na marafiki zake?
Maana upande wa pili wameamua kuungana nchi 59.
Hata hivyo,je unaweza kafananisha au kulinganisha msaada anaopewa Urusi wa kupelekewa askari 12000 kutoka Korea kaskazini ukilinganisha na misaada anayopewa Ukraine kutoka west?
Kwa mfano kwa uwazi kabisa Ukraine anapewa silaha mafunzo intelijensia fedha huduma za satellite na Kila anachotaka.
Hizo sio blabla bari wote hua tunaona vikao vya NATO vinavyokutana na kujadili namna ya kuisaidia Ukraine na pia hua tunaona utekelezaji wake,tumeshuhudia silaha zikiingizwa kutoka west kwenda Ukraine,tumeshuhudia wakufunzi,wataalamu,wanajeshi na mamluki wa west na NATO wakiwa vitani na wakiuliwa huko vitani.
Sasa wewe ukiondoa hicho kihabari chako niambie ni lini nchi marafiki wa Urusi zilikaa na kupanga kuisaidia Urusi kwa Kila kitu kama vile wafanyavyo west na NATO.?
Niambie ni lini china ama Iran ama Korea kaskazini walikaa na Urusi na kupanga na kutekeleza kwa kuipa Urusi silaha, intelijensia,huduma za satellite,fedha, ushauri,mafunzo na wanajeshi.?
Nitajie na aina ya silaha ambazo Urusi walipewa na nchi hizo hata kwa Majina,ukiondoa droni za Irani ambazo kwa hakika naamini Iran alitaka kuzijaribu TU,kwa Sababu Urusi hawakua na shida wala uhaba wa droni,Urusi walikua nazo kitambo TU.
Naomba unitajie silaha za marafiki zake Urusi walizompatia Urusi,kwa sababu marafiki zake Ukraine yaani west silaha zao zote tunazijua
Kwa uchache TU ni Himers,juveline,storm shadow, ATACMS, Patriot, Abrams, challenger, leopard, F-16, bushmasters,drone za Uturuki na silaha nyingine nyingi za aina tofauti kutoka nchi za west na zile zilzoKua Wanachama wa Warsaw Pact na zile zilizokua kwenye umoja wa USSR,mfano ndegevita,mizinga ,vifaru, makombora,ADS, melivita,boti n.k.
Kwa uchache ni hizo na nyingine nyingi Mimi na wewe tumeshuhudia zikichomwa na wanajeshi wa Urusi.
Sasa naomba nawe unaitajie Misaada aliyopewa Urusi kutoka kwa marafiki zake na uniambie ilianza kupelekwa Urusi lini,maana hao wanajeshi wa Korea kaskazini taarifa Yao umeiweka humu tarehe 18-10-2024 wakati vita ilianza tarehe 24-2-2022,bado miezi minne TU iwe imetimia miaka mitatu kamili.
Miaka mitatu yote Urusi imepigana na west wote bila wanajeshi 12000 wa Korea kaskazini.
Ndugu yangu KP, Urusi inapigana ikiwa imewekewa vikwazo kuliko nchi yoyote hapa duniani,Urusi inapigana na nchi ya Ukraine inayosaidiwa na umoja wa kijeshi wenye nguvu kuliko jeshi lolote hapa chini ya jua.
Tunaamini sayansi zote zimeanzia Ulaya,na ulaya ndio iliizaa Marekani na Marekani ndio taifa lenye jeshi namba moja duniani na Marekani ndio baba wa NATO na ndani ya NATO yumo UK , France, German,Canada, Denmark, Poland, Spain,Holland,Latvia, Estonia,n.k,Hawa wote Kwa umoja wao hata china na Urusi zikiunda jeshi lao la pamoja,kwa bajeti ya kijeshi hawaifikii uss
na USA na westnato.
Sasa Leo hii,hao wote akina NATO Urusi anapambana nao wote Kwa miaka mitatu na kawamudu.
Hawa NATO waliweza kumpiga Gaddafi, Saddam na Osama bin laden na Slobodan Milosevic.
Je Kuna ubaya Gani Urusi akisaidiwa wanajeshi na Korea kaskazini'?
Kama NATO Wana marafiki zao kwani Urusi Hana haki ya kua na marafiki?
Je Urusi imezidiwa kiasi kwamba bila msaada wa wanajeshi 12000 wa Korea kaskazini haitoboi?
Hivi hujasikia Urusi imepeleka silaha Iran na Ina wanajeshi Syria?
Je hiyo ndio nchi ya kutegemea wanajeshi 12 elfu wa KK?
Je NATO wanapenda kupigana vita na nchi zisizo na washirika?
Ndugu yangu nakuomba usifananishe misaada anayopewa Ukraine na marafiki zake dhidi ya misaada anayopewa Urusi na marafiki zake.
Ukraine anapewa misaada mikubwa mno,silaha alizopewa Ukraine wenyewe wanaozitoa wamelalamika zimeisha kwenye akiba zao.
Hatujasikia hata siku moja Urusi akilalamika kaishiwa akiba ya silaha,ndio kwanza wanatamba kua wanazalisha silaha mara Tatu kuliko nchi za west.