LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
JD ni mchonganishi sana, ukiangalia kiundani yeye ndo kama amesababisha hii vita ya leo, Trump kama alikua na staha fulani ya kiutu uzima ila Vance alikua anajitahidi sana kumchokonoa Zelensky mpaka nae busara ikamshinda akaamua kuanza kuropoka, na upande wa pili alijua kabisa kuna vitu akiongea lazima mashetani ya bosi wake yapande.

Unaweza sema walipanga makusudi kuionesha dunia Zelensky ni mtu wa aina gani make kete zilikua zinasukumwa kwa akili nyingi si mchezo.
 
Vance kachomekea eti Zele Oktoba mwaka jana alikwenda US akasaidia kampeni ya Kamala. Nadhani hii ndio chanzo cha hasira zao kwa Zele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…