SPEECH YA "CAPTAIN FANTASTIC" ILIYOBADILI MCHEZO 2005

Spav V

Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
11
Reaction score
52
Manuel Enrique Mejuto Gonzalez alizaliwa tarehe 16 aprili 1965 huko la Felguera Langreo,Hispania......Huyu ndiye mwanaume aliyechezesha mchezo wa finali ya klabu bingwa ulaya mwaka 2005 kàti ya Liverpool ya England na Associazione Càlcio Milan (Ac Milan) ya Italia.Katika kipindi chake çha uamuzi wa soka alichezesha mechi 37 za klabu bingwa na mechi 3 za kombe la Uefa.

Ndani ya dimba la Ataturk stadium Instanbul Uturuki mbele ya mashabiki 69,600,ndipo "greatest comeback" kuwahi kutokea katika miçhuano ya ligi ya màbingwa Ulaya ilifanywa na Liverpool ya Harry Kewell na Djimi traore dhidi ya Ac Milan iliyotimia "world class" players.
Ac milan çhini ya King Carlo walitumia mfumo wa 4-3-1-2 Dida golini,Maldini,Nesta,Stam & Cafu katika ulinzi,Kiungo àlikipiga Andrea Pirlo,Gattuso & Seedorf huku Kaka akitumika kama kiungo mshambuliaji nyuma ya Andryl Shevchenko na Hernan Crespo aliyekua anakipiga kwa mkopo àkitokea Çhelsea.
Liverpool chini ya Rafa Benitez walitumia 4-4-1-1 Dudek golini,Finnan,Traore,Caragher na Hyypia katika ulinzi,Captain Gerrard,Alonso na John Arne Riise katika safu ya kiungo huku Kewell àkiçheza nyuma ya Milan Baros.

Magoli ya Maldini dakika ya 1 ya mchezo nà mawili ya Crespo dakika ya 39 & 44 yalifanya ubao usomeke Ac milan 3:Liverpool 0 hadi kipindi cha kwanza kinaisha.

Djibril Cisse anatukumbusha speech fupi àliyoitoa "Captain Fantàstic" Steven Gerrard ambayo ndio inaàminika kubadili matokeo,Gerrard àlisema "Mimi ni mtoto wa Liverpool,muda wote nimekua katika klabu hii,sihitaji kuiona liverpool katika hali ilinayo sasa,ikionewa kiasi hiki,kwahiyo tukipata goli dakika 15 za mwanzo hakika tutashinda mechi".

Kabla kipindi cha pili kuanza Steve Finnan aliyekua beki wa pembeni àlimpisha Dietmar Hàmman na hii ilimaanisha mfumo ulibàdilika na kuwa 3-5-2 Riise na Smicer katika flanks,Alonso & Hamman kama Holding midfielders na Gerrard kama attacking midfielders.Dakika ya 54 Mr Liverpool àliipatia Liverpool goli la kuongoza huku Smicer àkifunga dakika ya 56 na Àlonso aliifanta 3:3 kwa kumalizia rebound baada ya penalty yake awali kupanguliwa ya Dida.

Meçhi iliisha 3:3 baada ya extra time na Liverpool ilishinda 3:2 kwa matuta baada ya Pirlo,Sheva na Serginho kukosa penati zao huku Riise pekee akikosa kwa upande wa liverpool.
Ukiacha miaka ya 1977 àmbapo liverpool ilichukua ubingwa back 2 back Liverpool iliendelea kuwa moto miaka ya 1981hadi 84,miaka hiyo ya 2000s pià Liverpool iliendelea kuwa moto sana tofauti na kipindi hiki ambapo Liverpool imepoa sana.
 
Shujaa ni Didi Hamann alivyoingia kipindi cha pili na kwenda kumfanya Andrea Pirlo asicheze na kuwarudisha Liverpool mchezoni
 
Umenikumbusha mbali,2007 kidogo historia ijirudie sema ikawa bahati mbaya
 
Dah, hongera sana. Hiii match niliiona kwa kiingilio cha Tsh.200 Sovi Songea. Ilikuwa Furaha sana kwa wapenzi wote wa time za england tofauti na akishinda Man au Chelsea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…