Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Hatuzungumzii kubambikizwa hapa bali njia halali wanazoweeza kutumia wanandoa kupata mtoto kama mmoja hana uzaziHakuna tofauti sana kati ya kutumia donated sperm kutoka sperm bank na mwanaume kubambikizwa mtoto.
Hope tuko wengi tunaotaka kujua hii kitu
Mzee yamekukuta nini? Wengine tunaweza kuchangia. Si mnaona hata majina yetu yalivyo.
Kenya ipo ila hapa TZ bado, si unajua hosipitali zetu siasa ni nyingi kuliko utalaamu. Mshikaji wangu alikwenda hospitali Nairobi na sasa wa mtoto wa mwaka mmoja na ushee na hakuna tatizo lolote kwenye familia kwani mshikaji ndiye mwenye tatizo. Hata familia yao wanajua na wamekubaliana na hali halisi.
Mhhhh! Msije kuwekewa mbegu bomu badala ya kutoka mtoto wa kimatumbi anatoka mtoto wa kihindi/kichina au kizungu inakuwa kizungumkuti kingine tena.
Mkuu sfm unakosea. Mbona yanazaliwa makinda yenye afya tu huko mahospitalini? Suala la udhibiti mbovu ndio nitakuunga mkono
Kuna mwana saikolojia mmoja alishawahi kusema, nature ya mtu pia hufuatana na afya aliyokua nayo mzazi wake..mfano,unapomuona mtu mbishi ama mkorofi kupita kiasi,na matatizo mengine ambayo huathiri ubongo kwa namna moja ama nyingine
Sikatai watoto wengi huzaliwa na afya nzuri,lakini ninachozungumzia ni ile afya ya saikolojia!
hivi kuna watu walioathirika kisaikolojia kama wazungu? They live in hell. We just dont know. Bado naamini tungekuwa na sperm banks ingepatikana michango bora kabisa ya mbegu. Siamini kama hao wadhibiti wangealika mradi mtu tu kuchangia. Lazima wangeangalia afya ya mwili na akili, umbo, uelewa etc. Tena wagumba wangepata mbegu bora sana