Spika akijiuzulu atapata hadhi ya Spika Mstaafu?

evangelical

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2011
Posts
5,035
Reaction score
8,218
Nafahamu kwamba spika akistaafu kwa kumaliza muda wake anapata marupurupu ya spika mstaafu ambayo asilimia 80 ya mshahara wa spika atakayekuwepo hadi atakapofariki, lump sum pensheni ya jumla ya mishahara wake aliopokea kama spkika,diplomatic passport .

Kwa subwoofer aliyejiuzulu itakuwaje?
 
Hakuna kustaafu kwenye siasa kuna kumaliza muda wako na njia moja wapo ya kumaliza muda ni hiyo aliyotumia Ndugai hivyo ana haki na hadhi ya stahiki zote.

Stahiki hizo ni haki ya yeyote aliyewahi kupata cheo cha spika hata kwa siku moja
 
Yes ndio maana waliokuwa wanamshauri ajiuzulu ili kulinda heshima maana yake atapata full benefits na hadhi ya mstaafu.maana angesubiri kufurushwa ingekula kwake.
 
Yes atapata Kama Lowassa anavyopata japo alijiuzulu
 
Spika aliyejiuzulu lakini najua watalazimisha aitwe mstaafu kama Lowassa.
 
Suala la lowasa kuitwa waziri mkuu mstaafu nao ni upumbavu uliopitiliza
Kujiuzulu sio kustaafu
 
MWACHE ALE MPUNGA WAKE TARATIBU
BILA KOKORO

ova
 
Hata Lowasa anapata kila kitu,Kwahiyo Ayubu ataendelea kupata stahiki hiyo
 
Ni Tanzania tu Hata UKIJIUZULU kwa KASHFA unaendelea Kuitwa MSTAAFU km Lowassa Sitashangaa hata NDUGAI akaitwa SPIKA MSTAAFU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…