Katika hali inayojionyesha nia ya kujenga himaya ya utawala kwa siku za baadae, Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania amemwaga kiasi kikubwa cha fedha mkoani Tabora ili kumsaidia kijana mmoja aitwaye Paul Shija ambaye ni katibu wake wa Jimbo anayegombea U-enyekiti wa UVCCM mkoa wa Tabora! habari nilizozipata muda si mrefu ni kuwa pamoja na mapesa hayo Spika anashirikiana na Ismail Aden Rage ambaye pia ni mwenyekiti wa wazazi Mkoa wa Tabora! Taarifa zaidi zinadai kuwa Spika Sita anasaidiana pia na Mkuu mmoja wa Mkoa jirani ambaye ni rafiki yake wa karibu, kwa taarifa hii niombe vyombo vya dola viwe macho 08/12/2008 siku ya J3. taarifa zaidi zinadai kuwa msafara wa wapambe upo njiani kutoka Dar kwenda Tabora ili kuhakikisha kuwa kijana huyo anashinda