Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amepotosha umma mchana kweupe kudai ajira za ualimu zilizopita zilitolewa kwa misingi ya kikanda na ukabila kwa sababu ukiachilia mbali jina moja lililojirudia kila ukurasa, mchakato wa ajira zilizopita ulifanyika kwa haki na kila mwenye sifa alipata nafasi ya kuajiriwa.
Pia soma > Spika Ndugai: Ajira ziwe zinazingatia usawa wa Kijografia
Katika hatua nyingine Job Ndugai anauliza wabunge kama wapiga kura wa majimbo yao waliajiriwa kwenye ajira zilizopita. Ebu tujiulize, wapiga kura anaowasema Job ndugai ni akina nani..? Je, ni watanzania? Kama ni watanzania walitokea wapi kama sio huko huko majimboni anakokusema spika Ndugai?
Je, Spika Ndugai ana majina mfukoni ya vijana wa jimbo lake waliompigania kwenye uchaguzi anaotaka kushinikiza waajiriwe?
Nauliza hivi kwa sababu kabla mchakato wa ajira kutangazwa baadhi ya wabunge walichukua majina ya vijana majimboni kwao kwa madai kwamba wanaenda kuwapigania wapewe kipaumbele cha ajira kwa kisingizio kwamba wanajitolea. Kwa hiyo inawezekana Spika Ndugai nae yupo kwenye kundi hili ndio maana anapiga kelele ili ajenda yake ifanikiwe.
Na, kama ajira zilizopita anasema zilikuwa zimegubikwa na ukabila mbona hakusema kipindi hicho anakuja kulisema hilo leo?
Kwa kipindi chote ambacho ajira zimekuwa zikitolewa enzi za magufuli spika Ndugai alikuwa kimya wala hatukusikia akiagiza kamati za kisekta kufanya uchunguzi lakini leo kwenye utawala wa Rais Samia anaibuka na kudai kamati hizo zifanye kazi yake. Je hiki ni kielelezo kwamba Spika Ndugai alimwogopa magufuli na anamchukulia poa Rais Samia?
Kimsingi kelele za spika ndugai zimebeba ajenda binafsi nyuma yake na kama Tamisemi watazisikiliza zitakuja kuharibu mchakato wa ajira kwa sababu kama yeye amekuja na kigezo cha ukabila, mwingine atashauri kigezo kiwe umri na mwingine anaweza kushauri kigezo kiwe ni rangi nyeupe, mwisho wa siku vigezo vinakuwa vingi kuliko ajira zenyewe.
Kwa hiyo ni vyema Tamisemi mkafanya kazi yenu kwa vigezo mlivyojiwekea ili kila mwenye sifa aajiriwe as long as amehitimu mafunzo ya ualimu na ana vyeti halali lakini kutaka kusikiliza kila anachosema mwanasiasa ndio kiwe mtakuja kuharibu mchakato mzima kwa sababu wanasiasa naturally ni wabinafsi ambao kazi yao kubwa ni kulinda maslahi yao hasa ya kibunge.