Spika Ndugai aache kupotosha umma kwamba ajira zinatolewa kwa upendeleo wa kikabila na kikanda

dini,kabila na maeneo atokayo mtu sio kigezo cha kupewa kazi au uteuzi, ujuzi,elimu na weledi ktk kazi ndivyo vinaamua, dini wakachuguane huko kwenye dini zao, na makabila huko wanakoenda kutambika. Tanzania haina dini wala haina kabila, Tanzania ni ya Watanzania wote.
 
Naunga mkono 100%
Sioni usahihi wa Spika kwenye hili, wabunge wanatofautiana ushawishi na uwezo wa kuzonga na kuzengea.Hi inaweza kupelekea baadhi ya wabunge wasio na ushawishi kukosa au kupata idadi ndogo kwenye majimbo yao,na wale ma veterani kwenye ushawishi kujizolea idadi kubwa kwenye majibo yao.

Bunge lilitakiwa kuhakikisha kuwepo kwa rationaleya mgao kwa majimbo yote.
Spika kushawishi wabunge wafanye lobbying ni kiashiria cha Bunge kupoteza mwelekeo.
 
...
Hilo Jambo limeanza leo? Yeye alikuwa wapi? Wakati jpm anateua viongozi wote wa vyombo nyeti toka Kanda moja yeye alikuwa wapi? Acheni unafiki.Aseme mwingine Sio spika ndugai
 
hakuna tatizo kama hawalalamiki, lkn kama wana lalamika ujue kuna tatizo lina nyemelea, jambo la msingi kama alivyo sema Spika ni kuweka mseto, nchi imara ni ile inayo jengwa na watu wote, wote wahisi hii ni nchi yao.

yaliyo semwa wakati ule na Mwalimu yali kidhi mahitaji ya kipindi kile sio nyakati hizi tena.
lazima viongozi wetu wabadilike haraka sana.
 
Ndugai akiwa kwenye siku zake anaongeaga point tupu.
 
...wakati unzidi spika wa bunge alikuwa nani
Alikuwepo palepale kwenye kiti chake cha enzi,
Lkn kutokana na mfumo wa utawala ulivyokuwa ni kuwa kila mtu alikuwa anakimbiza bawa lake ili maisha yasonge.

Leo hii tunamuona mama Samia akiyakataa yale yote yaliyokuwa yanakubalika kipindi cha awamu ya 5 na yeye alikuwa mwana familia ya hiyo awamu.
 
Yeye mwenyewe tu ameingiza wabunge feki bungeni, huo uhalali wa kuhoji watumishi kwenye kada zilizotangazwa anapata wapi?

Sawa kabisa, yeye Ndugai na wabunge wenzake wa ccm waseme wameingiaje bungeni, mpaka yeye leo aweze kuhoji weledi wa taasisi nyingine.
 
Haahaa
Unafiki mtupu....
 
Sawa kabisa, yeye Ndugai na wabunge wenzake wa ccm waseme wameingiaje bungeni, mpaka yeye leo aweze kuhoji weledi wa taasisi nyingine.
..kushangilia kinachosemwa na ndugai Ni kukosa weledi wa mambo
 
...
Huo mseto umuhimu wake unaonekana leo? Spika alikuwa wapi wakati Jpm anaweka watu toka Kanda moja?
 
Hawa wote yani Ndugai na TAMISEMI wote wana matatizo hasa TAMISEMI kuna figisu sana kwenye suala la ajira upendeleo na vimemo ndio kinachoendelea pale kwa hiyo huu msuguano unazidi kutuonyesha sisi wananchi sarakasi zilivyo huko lakini tukumbuke tu kuwa nafasi mlizonazo sasa hivi ipo siku mtatolea hesabu kwa Mungu hii nchi ni yetu sote hivi tukiendekeza upendeleo kiasi hiki je watoto wa masikini wasio na watu wao TAMISEMI au kujuana na watu watu wakubwa kama spika ina maana hawatapata ajira? je kama hawatapa ajira hamuoni manawaumiza?
 
Hata kama wanalalamika wanatakiwa wajue ukweli, huwezi kupewa kazi au cheo kwa sababu ya dini,ukabila au ukanda. kwani watu wataanza kulalamika huduma mbovu, maendeleo hakuna na uonevu. kama we ni wa dini nenda kafanya kazi kwenye dini yako, kama ni kabila kahudumia mizimu na kutambika kama unataka Ukanda baki nyumbani kwenu ukiangalia milima na mabonde. kama ni kazi ya serikali lazima uwe na Elimu, ujuzi na weledi
 
Ukiangalia kwa jicho la Tatu Ndugai yupo sahihi kabisa.
Sahihi kuanzia lini? Alikuwa wapi miaka Mitano iliyopita, ambayo ilikuwa imejaa Kila Aina ya injustice. Anatoa wapi moral authority kusema hayo wakati yeye mwenyewe ni unjust. Unakataliaje wabunge ambao wamefukuzwa kwenye chama Chao kwa sababu ya irreguraties walizocheza na unawapa haki kinyume Cha Sheria za nchi.
Uliona wapi Ndugai akiwa mtu mwenye haki na sober?
Apuuzwe!
 
Ndugai angalia na kutunza ulimi. Ya bandari Bagamoyo hatujasahau umeanza ajira za ualimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…