Spika Ndugai aache kupotosha umma kwamba ajira zinatolewa kwa upendeleo wa kikabila na kikanda

Ndugai ni spika wa hovyo kabisa asipo angaliwa vizuri atasabisha chuki kubwa sn
Ajira zilikuwa zinaangalia watu wa kanda ya ziwa,,

Kwaiyo ndugai yupo sahihi,,, dikteta aliharibu Nchi
 

Spika aboreshe shule za Kongwa kwanza ili awe na kigezo cha kulalamika. Huyu spika mlimtolea wapi?
 
Utumishi wa umma ni Dhamana tu sio mali ya mtu binafsi au kampuni ya mtu binafsi.

kuna baadhi ya viongozi wanajisahau sana wana dhani kuwa kiongozi ndani ya utumishi ni sawa na kumiliki kampuni yako binafsi na hivyo unaweza kumuweka mtu unaye jisikia au kumpenda na kumuacha usiye mpenda.....hapana!.

unaweza kufanya hayo endapo tu una miliki kampuni yako binafsi lkn sio ktk utumishi wa umma.
 
Ukiangalia kwa jicho la Tatu Ndugai yupo sahihi kabisa.
Usahihi wake uko wapi kwa sababu ukichunguza vizuri hoja aliotoa utagundua ana jambo lake analotaka lifanikiwe. Kwa kuthibitisha hilo leo bungeni amekataa wazi wazi walimu wa kike kupewa kipaumbele cha ajira. Maana yake nini kama sio kuwa ana majina yake mfukoni anayotaka yapewe kipaumbele?
 
Nafasi hitajika ni 6000 waombaji wenye sifa ni zaidi ya 700,000 iv kwann serikal isirejeshe mazingira mazurinya private sectors kujazilizia uhaba wa ajira
 
Ajira zilikuwa zinaangalia watu wa kanda ya ziwa,,

Kwaiyo ndugai yupo sahihi,,, dikteta aliharibu Nchi
Huku ni kujishuku upumbavu tu.

Magu hakuwahi kupendelea watu wa kanda ya ziwa wala wasukuma.

Magu alikuwa na genge lake maalum alilotoka nalo wizara ya ujenzi hasa TANROADS ndio alikuwa anakomaa nalo.

Watu wake wengi wa karibu siyo watu wa kanda ya ziwa.
  • Mfugale
  • Kijazi
  • Kabudi
  • Ndugai
-

Na mnaposema kanda ya ziwa mnaijua vizuri, ni mtu gani alikuwa na ukaribu na Magu kutokea Mara ?
 
Hata nami namuunga mkono maana ukanda ulizidi sana kila kitu ilikuwa ni masanjah
Sikatai ukanda ulikuwepo kwenye nafasi za uteuzi lakini kwenye ajira za utumishi wa umma hapakuwepo upendeleo wowote, watu waliajiriwa kwa usawa. Kwa hiyo hoja yako ya ukanda unataka kutuaminisha kwamba ajira zilizopita waliajiriwa wasukuma au watu wa kanda ya ziwa tu?
 
Sikatai ukanda ulikuwepo kwenye nafasi za uteuzi lakini kwenye ajira za utumishi wa umma hapakuwepo upendeleo wowote, watu waliajiriwa kwa usawa. Kwa hiyo mnataka kuniambia ajira zilizopita waliajiriwa wasukuma tu?
Ni 60%
 
Kwa ujumla, binadamu hatustahili kufurahia kifo cha mwanadamuwenzetu awaye yeyote.

Mimi sifurahiibkifo cha Mwendazake lakini nimefurahia sana kuondoka kwake kwenye nafasi ya Urais. Maana kama angeendelea, sijui huko mbeleni kungetokea nini!!

Alikuwa ameanza kupandikiza mbegu mbaya ya ukabila, ukanda na undugu. Ukuaji wa uchumi alikuwa anaudondosha kwa kasi ya ajabu.
 
Alichosema Job kina ukweli sana tu.

Mfano ni wizara ya Afya,alivyokuwepo Ummy mwalimu,watu wa Tanga wengi wamepata shavu sana.

Mfano tu baraza la wafamasia.Watu waliopata scholarship wakati wake kutoka Tanga ni wengi.
Wapare nao wameingia kwa kasi ya ajabu.
Kifupi tu ni kwamba ubaguzi wa jinsi hii ulianza kuthaminiwa wakati wa JK na ukapigwa muhuri wakati wa JPM.
Sasa mama wanampima imani.
 
Kwa ratio hiyo sioni tatizo hapo. Kumbuka kanda ya ziwa ndio kanda yenye mikoa mingi na watu wengi kwahivyo ata namba ya wahitimu lazima iwe kubwa kulinganisha na kanda zingine.
 
Kama aliyaishi na kuyashuhudia mbona hakuyasema kipindi cha mwendazake?
Ndo mjue spika ana ajenda yake iliyojificha nyuma ya hizi ajira
 
Kwa ratio hiyo sioni tatizo hapo. Kumbuka kanda ya ziwa ndio kanda yenye mikoa mingi na watu wengi kwahivyo ata namba ya wahitimu lazima iwe kubwa kulinganisha na kanda zingine.
Jiwe alikuwa mbaguzi sana
 
Kama aliyaishi na kuyashuhudia mbona hakuyasema kipindi cha mwendazake?
Ndo mjue spika ana ajenda yake iliyojificha nyuma ya hizi ajira
Ndani ya ccm bado hakuna msafi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…