Spika Ndugai aache kupotosha umma kwamba ajira zinatolewa kwa upendeleo wa kikabila na kikanda

Kwa ratio hiyo sioni tatizo hapo. Kumbuka kanda ya ziwa ndio kanda yenye mikoa mingi na watu wengi kwahivyo ata namba ya wahitimu lazima iwe kubwa kulinganisha na kanda zingine.
Unachoongea siyo kweli. Walimu hawapigiwi kura bali ni qualification.

Random sampling:

Wanafunzi wa vyuo vikuu kwa miaka mingi:

1) Kagera
2) Kilimanjaro
3) Mbeya
4) Iringa

Uwiano huo huo unauona kwa wakufunzi.

Kwenye population, mikoa ya kanda ya Ziwa ina-count 10% ya population yote.
 
Kwenye hili kama hujamuelewa Ndugai utakuwa na chuki zako tu binafsi, huyu Mzee sijawahi kuwa kwenye mstari wake ila aliyosema ni mnufaika wa hizi dili za ajira ndio ataona Ndugai anabutua mpira wao. Tunajua na ushahidi upo ajira hizi zilikuwa tayar zishapata watu kabla ya maombi na hapa kuna kundi la wahuni walikuwa wanaenda kujaza vijana wao wa kusifu na kuabudu.
 
Kwa wabunge ndio wapeleke watu wa kuajiriwa? Je namna ya kuwapata huko kwenye majimbo yao, utaratibu upo? Hapa sio kuzalisha tatizo juu ya tatizo. Na je, taarifa za wanaofaa kuajiriwa toka kwenye majimbo ziko wapi? Kati ya jambo la hovyo ni hili. Athari zake ni kubwa mno ikiwa ni pamoja na kuruhusu rushwa kutembea zaidi. Kazi ya bunge ni kutunga sheria na kusimamia serikali. Haya ya kupeleka waajiriwa ni ujinga mwingine wa bunge letu.
Nchi iongozwe kwa taratibu, na taratibu za kuajiri watu zipo. Haya mambo ya maeneo haya yakiendelezwa muda si muda tutaibua vita ya kikanda ama kijimbo. Tuache vigezo vilivyopo vitumike na anayevifikia apate ajira. Kama vina kasoro basi virekebishwe, nje ya hapo kuna janga kubwa linainyemelea nchi.
 
ndugai anaumwa pale tu bungeni anawabunge fake aliowaingiza kilaghai sasa anauhalali gani kuzungumzia hayo
 
...

Huo mseto umuhimu wake unaonekana leo? Spika alikuwa wapi wakati Jpm anaweka watu toka Kanda moja?
Wewe kipindi JPM anafanya hayo uliyaona na je ukikuwa na ujasiri wa kuyasema hadharani achilia mbali hapa nyuma ya keyboard? Kila jambo na wakati wake na kukwepa hatari ni bora kuliko kuikabili bila silaha kwa kigezo cha ujasiri.
Kuna muda inabidi umpe adui nafas akushambulie ila ukiibuka unampasua vizur kabisa.
Muache Ndugai na wenzake waseme yaliyojificha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…