Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,710
- 9,063
Sakata linaloendelea kati ya Spika Ndugai, CHADEMA na wale Wabunge 19 waloapishwa kinyume cha Katiba ni aibu kwa Tanzania.
Ili kukomesha huu upuuxi wa Spika Ndugai CHADEMA lazima ifungue kesi Mahakamani haraka sana ili sheria ichukue mkondo wake.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko wazi kabisa kuhusu mchakato wa uteuzi wa majina ya Wanawake wa Viti Maalumu toka chama chochote cha siasa chenye usajili halali. Spika Ndugai anajua hili na hata Rais Magufuli anajua hili. Lakini pia CCM, Jaji Mkuu, DPP na IGP wanalijua hili.
Kwamba ili Mbunge aingie Bungeni iwe ni kwa kuchaguliwa, kuteuliwa au Viti Maalum LAZIMA AWE MWANACHAMA WA CHAMA CHA SIASA KILICHOSAJILIWA kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya kinamama 19 wa CHADEMA kuvunja Katiba ya CHADEMA kwa kukiuka Sheria na Taratibu za Uteuzi wa Viti Maalumu kwa kujipa mamlaka ya kujipendekeza, kujiteua na kuwasilisha majina yao kwa Spika, Kamati Kuu CHADEMA iliwaita kuwahoji lakini wakakataa wito huo na hivo kupelekea KK-CHADEMA kuwatimua uanachama na hivo kupoteza sifa ya kuwa Wabunge wa Viti Maalumu.
Kwa akili za kijinga kabisa Spika ameamua kuwatetea hawa Wanawake 19 aliowaapisha akijificha kwenye kichaka cha kutetea Wanawake. Ndugai amesikika akisema hatakubali kina Mdee wavuliwe Ubunge wao maana ni uonevu Ndugai amehoji swali la kipuuzi kabisa ati Mbowe ni nani Nchi hii
Ndugai anajifanya hajui kuwa Mbowe ni Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA ambacho hao wanawake 19 aliowateua na kuwaapisha wametoka kama haitoshi Spika amemlaumu Mbowe kwa kunyanyasa wanawake haohao ambao waliumizwa kwa kuvunjwa mbavu,mikono na miguu na Polisi kwasababu ya Mbowe. Jeshi la Polisi ya CCM ndiyo walohusika na unyama huo lakini Ndugai anatupa lawama kwa Mbowe.
Bado Ndugai ametoa madai mazito kuwa Mbowe hataki hao Wanawake 19 waingie Bungeni kwa vile siyo vimada au wapenzi wa Mbowe au Mnyika. Huu ni udhalilishaji(defamation) kwa Viongozi wa CHADEMA.
Nawashauri CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti Mbowe na Makamu wote 2 Tundu Lissu na Salimu Mwalimu wafungue kesi haraka sana Mahakamani kama ifuatavyo:

- Kupinga uteuzi wa Wanawake 19 kuwa Wabunge Viti Maalumu ilhali sio Wanachama wa CHADEMA.
- Kumshtaki Spika Ndugai kwa kuvunja Katiba ya nchi akilazimisha kuwatambua Wabunge Viti maalumu wasio wanachama wa CHADEMA.
- Kuwadhalilisha Viongozi wa CHADEMA kwa kudai kuwa wanajihusisha na Rushwa ya Ngono ndani ya Chama.
- Mwenyekiti Kaijage na Mkurugenzi NEC kwa kughushi barua na majina ya hao wanawake 19 na kupeleka kwa Spika.