blackstarline
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 3,278
- 7,966
SPIKA NDUGAI APUUZWE TU
Tatizo la Tanzania ni Bunge kutaka kuwa juu ya Mihimili mingine. Kikatiba, watu wenye akili na mitazamo za kindugai wanatafsiri vibaya, si kwamba kuisimamia serikali ni kuilazimisha kufanya matakwa ya bunge.
Kauli ya Spika Job Ndugai kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi kusema anataka wabunge wote watokane na CCM ili kukidhi akidi ya bunge kufanya maamuzi wa yale yanayojadiliwa ni ya ukiukwaji na ameonyesha jeuri na kiburi cha nafasi aliyonayo.
Unaweza kupata picha ya kwa nini akina Paul Makonda na Stephen Masele wameshindwa kuteuliwa katika uchaguzi wa ndani ya chama, watu wanaweza kusema labda Makonda kwa sababu yake ya kuanzisha vita dhidi ya wauza madawa ya kulevya pekee waliwekeza nguvu nyingi pale Kigamboni ili kumwangusha, wakijua akipita huenda akawa waziri atayehusika na mambo haramu.
Lakini kwa kauli ya Ndugai kutokana kabisa wapinzani washinde uchaguzi huu, inaonyesha hata wale wana CCM ambao hawakubaliani na mambo yake ya udikteta bungeni, amewashughulikia ili asipate taabu katika uendeshaji wa shughuli za bunge.
Huko ndiko kuingilia mihimili mingine, kauli ya Spika Job Ndugai ilipaswa kutolewa na viongozi wa vyama vya siasa hususan CCM na vyama vingine maana kila chama kinataka kushinda uchaguzi katika kata na majimbo yote, lakini sio mkuu wa mhimili mmoja kuingilia mhimili mwingine.
Mazoea haya yakiachwa yaendelea bila kukemewa, yataota mizizi katika jamii kwenye Mihimili ya nchi kama ilivyofikia katika vyama vya siasa, si kwa Chadema wala CCM demokrasia ya ndani na vyama hivyo imezalisha madikteta.
Dkt John Pombe Magufuli pamoja na misimamo yake, kwa yalimtukia ndani ya chama akiwa mwenyekiti tangu uchaguzi wa ndani 2017 na huu wa 2020, ameshaonyesha kusareda na kilichobaki ni kutimiza majukumu yake ya kiserikali pekee.
Lakini mwisho wa kupuuzia mambo ya msingi katika kuyashughulikia matatizo huwa si mzuri, kunaweza kutokea anguko kubwa sana, iwe ni kwa kupitia wananchi au Jeshi lenyewe, maana maumivu yana mwisho wake.
Tunaweza kuyafumbia macho madhaifu ya kisiasa kwa viongozi wa chama kushindwa kuja na sera, falsafa kwa aibu ya kujibu hoja za wapinzani au wananchi kwa kuwaondoa katika ushindani kwa kuficha aibu ya kushindwa kwa chama, lakini matokeo yake yanaweza kuwa hasi zaidi kwenye jamii viongozi kukosa furaha na uhuru wa kuongoza.
Hata kesho ya chama kuwa si nzuri sana kama tunavyojipa matumaini.