Spika Ndugai atatizwa na tafsiri ya Katiba, aamua kumruhusu Dkt. Mpango kuwaaga wabunge wenzake kabla ya kuthibitishwa na Bunge

Spika Ndugai atatizwa na tafsiri ya Katiba, aamua kumruhusu Dkt. Mpango kuwaaga wabunge wenzake kabla ya kuthibitishwa na Bunge

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Spika Ndugai amekiri kupata wakati mgumu kwenye kuitafsiri Katiba iwapo Dkt. Mpango awaage wabunge wenzake kabla ya matokeo ya kura kutangazwa na kumthibitisha au baada yake.

Amesema iwapo atamtangaza Dkt. Mpango amepitishwa kuwa Makamu wa Rais basi haitawezekana tena mteule huyo kupewa fursa ya kuongea kwani atakuwa siyo Mbunge tena.

Na iwapo atampa fursa ya kuliaga bunge kabla matokeo ya kura hayajajulikana nayo ni kama haijakaa sawasawa.

Lakini mwisho Spika Ndugai ameamua Dkt. Mpango aliage Bunge kabla ya matokeo kutangazwa.

Maendeleo hayana vyama!
 
Busara imetumike cha msingi wampe kura za ndioooooooo kama zote. Baada ya hapo katiba irekebishwe kwa kuzingatia hili lililojitokeza leo.

Katiba haiwezi kamilika na kujitosheleza wakati wote hadi kunapotokea utata kama huo ndipo marekebisho yanapoonekana kuhitajika
 
Hivi Mpango si mbunge mwenye Jimbo?

Hii imekaaje pia, jimbo linaachwa wazi kimasihara hivi..
 
Sasa nimejua why WALE 19 wapo bungen.


#EMPOWERwomen.
 
Back
Top Bottom