Spika Ndugai awaapisha Humphrey Polepole na Riziki Lulida. Asema Bunge linawatambua Wabunge 19 wa Viti Maalum waliofutiwa uanachama CHADEMA

Wameapishwa GEREJI hahahaa.
 
Ndio siasa! Mbona nyie mlikuwa mko tayari kuua mtu ili mradi kumtetea Mdee ila leo mnamuita mzee?

Pia umesahau ya Lowasa? Haya yanayowapata Chadema ni halali yenu.
Two mistakes can't make one right.

Kuwa na akili japo za kuazima kwa huyo mtoto alie karibu yako apo.
 
Bunge halina uwezo kisheria kuendelea kuwa na covid19 Bungeni. Kwa Sheria ipi? Ndugai aache hoja za kitoto. Hili si Bunge la kongwa.
 
Mkuu MtamaMchungu , kutafsiri sheria, legal interpretation ni a specialised field na haifanywi na kila mtu, ndio maana kwa Tanzania inafanywa na mahakama kuu pekee. Katika kutafsiri sheria, au katiba, kitu cha kwanza cha kuzingatia ni mtunga katiba alidhamiria nini kwa kifungu hicho.

Nimeonyesha mtunga katiba alidhamiria Mbunge ataapishwa Bungeni mbele ya Spika, kitu muhimu ni Bungeni, kwa maana ya kikao cha Bunge na sio jengo la Bunge!.

Kikao cha Bunge kinaweza kuitishiwa popote sio lazima ndani ya jengo la Bunge, kitu muhimu ni kikao na sio Spika.

Bunge ni jengo tuu, lakini kikao cha Bunge ni zaidi ya jengo. Mbunge anapaswa kuapa Bungeni mbele ya Spika Kanuni hiyo imempa Spika mamlaka ya kujingeuza yeye ndio Bunge hivyo popote atakapochagua, hata hiyo car park kuwa ndio Bunge!. This is wrong!.

Jengo sio issue, popote kunaweza kufanyika kikao cha Bunge hata hapo gereji, lakini essence ya kiapo cha Mbunge ni Bungeni mbele ya Spika.

Ni kama ilivyo Ikulu, ni makazi yoyote ya rais wa JMT anapoweza kufanyia majukumu ya kiurais, hivyo hata rais anapokuwa mapumzikoni Chato, akifanya jukumu lolote la urais, then hapo Chato panageuka ni Ikulu ya Chato!.

P
 
Wakati anachukua ile fomu moja tu iliyokuwepo chamani kwake ya kuteuliwa kuwania urais tulichukulia poa. Kosa kubwa la kiufundi. Iliandikwa kwa herufi kubwa: KUONGOZA VYOMBO VYA DOLA. Sasa ndio tunashtuka?
 
Katika sakata la Chadema,spika amekiuka katiba. Chama chochote cha siasa hapa nchini hata iwe ccm kikimkataa mwanachama wake hakuna mamlaka inayoweza kubatilisha zaidi ya mahakama.

Hao wanaoitwa wabunge wa viti maalum kutoka chadema kama hawaridhiki na maamuzi ya kamati kuu ya chadema wadai haki zao kwa mujibu wa katiba na siyo wewe kusimama kuwakingia kifua.Wabunge wangapi walifukuzwa katika vyama vyao na wewe ukawatetea? Kwanini uwe mtetezi kwa hao wa chadema?
 
Wakati anachukua ile fomu moja tu iliyokuwepo chamani kwake ya kuteuliwa kuwania urais tulichukulia poa. Kosa kubwa la kiufundi. Iliandikwa kwa herufi kubwa: KUONGOZA VYOMBO VYA DOLA. Sasa ndio tunashtuka?
Ngoja tuendelee kuisoma no
 
Mh Spika jana kaongea mambo mazito kuhusu CHADEMA na Mbowe kwenye suala la viti maalum. Kasema yanayofanyika kwenye hivi vyama ni ya kusikitisha na kutisha. Kaendelea kusema kuwa baadhi ya vyama ni kama SACCOS na ni kampuni binafsi za watu.

Kasema kuwa watu ni miungu watu na kwa uwazi kamtaja Mbowe kuwa anaendesha chama kwa upendeleo huku akiwapatia viti maalum watu special. Tena kasema kwani yeye anadhani ni nani kwenye nchi hii?

Sasa swali langu ni hili, iwapo haya yote ni kweli yanatendeka, kwanini hatua madhubuti za kisheria hazichukuliwi dhidi ya wahusika? Mbona inakuwa ni kupashana zaidi?

Na sasa najua mipasho itahamia bungeni hapo february, sasa haya mpaka lini?
 
It is clear, Tanzania nowdays is like a family of one unfocused man, who orders what he wants to be done!

No freedom of speech and expression

No constitutional law anymore

Katiba inakanyagwa Kwa maslahi ya wachache, watanzania nikiwemo na mm tumefungwa tungali tunatembea!
......God....have mercy on us....!
 
Ndio ishageuzwa kuwa hivyo. Kwa sasa bunge maana yake spika. Halafu kwa sasa bungeni ni eneo lote la bunge sio lazima ndani ya bunge .
 

Mpaka pale wananchi tutakapoamka na kuirejesha nchi yetu mikononi mwetu, dhidi ya wanaodhani kuwa wanatumiliki sisi na nchi kama mali zao.
 
Mpaka pale wananchi tutakapoamka na kuirejesha nchi yetu mikononi mwetu, dhidi ya wanaodhani kuwa wanatumiliki sisi na nchi kama mali zao.
NCHI iko salama ndiyo maana umeweza kuandika ulichoandika tofauti na upande unaoshabikia

Ushauri kwako na wafuasi wenzio wa "Mwamba tuvushe" kama ambavyo viongozi wake wanavyomsujudu, ninyi mnamwogopa humu JF kumwambia ukweli kuwa Chama siyo SACCOS.
 
NCHI iko salama ndiyo maana umeweza kuandika ulichoandika tofauti na upande unaoshabikia

Ushauri kwako na wafuasi wenzio wa "Mwamba tuvushe" kama ambavyo viongozi wake wanavyomsujudu, ninyi mnamwogopa humu JF kumwambia ukweli kuwa Chama siyo SACCOS.

Nasema uongo ndugu zanguuu.... uu...uuuuu?
 
Naunga mkono hoja masuala ya Tanzania kuzungumzwa Tanzania na siyo nje. Tutatue matatizo yetu wenyewe. TUJITEGEMEE.
 
Hongera sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…