Spika Ndugai: Kamati za Bunge zisikae tu bila kufuatilia mambo

Spika Ndugai: Kamati za Bunge zisikae tu bila kufuatilia mambo

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amezitaka Kamati za Bunge hususani zile za Sekta kufanya kazi zinazohusika nazo akisema zisikae tu pasipo kufuatilia mambo.

Ametolea mfano suala la Ajira za Walimu ambapo amehoji, "Wangapi mnajua Wapiga Kura wenu wangapi wamepata? Mnaweza kuwa na uhakika mchakato huo umekwenda inavyopaswa?"

Ameongeza, "Tusipoangalia tutajikuta katika Nchi hii badala ya Utumishi wa Umma wa Watanzania wote, tukawa na Utumishi wa baadhi ya watu. Hatuwezi kwenda hivyo".
 
Mfano Jimbo la kongwa ajira zilizopita, hakuna hata kijana mmoja alipata nafasi hizo. Kuna uwezekano ajira zote zikatolewa au kutokea kwenye mikoa milwili au mitatu tu, wakisingizia mfumo wa ajira.
 
Hawana uwezo wa kufuatilia kwa sababu Wengi hawana Elimu,ujuzi na uzoefua wa kufanya hizo kazi
 
Sawa ndungai kuna halafu ajira zote zinaweza kwenda kisiwa maarufu.
 
Spika ndugai ni miongoni mwa viongozi wachache duniani waliobarikiwa nguvu nyingi kuliko akili.
 
Back
Top Bottom