kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Nimekusikia Spika Ndugai ukisema kina Mdee, Bulaya na matiko wameteseka kwa ajili ya Mbowe halafu Mbowe anawafanyia hiyana kwa kuwafukuza chama ili watoke bungeni. Eti Mdee alivunjika mkono kwa kumtetea Mbowe.
Nimeshangaa sana huo uzalendo wa hao kina mama inawezekana ni kwa mahaba ya mapenzi au uzalendo wa ki Chadema usiyokua na maana kwa wana CCM na serikali yao.
Chadema wanapigania kitu wanakijua wenyewe ambacho ni hatari kwa wana CCM. Wanapinga ujamaa na kujitegemea na wanaunga sera za ubinafsi za kiliberali za Ulaya ambapo kwa sisi afrika zinatoa mwanya kwa ufisadi dhidi ya mali ya umma rushwa na dhuluma kwa wanyonge. Wanapinga kupigwa vita rushwa mahakamani eti ni kuingilia uhuru wa mahakama.
Ndugai asijitakie lawama kwa kuingilia mambo ya ndani ya CHADEMA. CHADEMA ni chama halali cha kisiasa nchini kina haki zake. Kama wamewafukuza wanachama wao uanachama ni haki yao na ni shauri lao. Hata kama waliofukuzwa ni wabunge ndugai kama speaker hana uwezo kuacha kutimiza wajibu wake wa kikatiba kwa kuwafukuza bungeni.
Katiba iko wazi hakuna mbunge anaweza kua mbunge bila kua mwanachama wa chama cha siasa. Kwa hivyo wajibu wa Speaker ni kuwatimua wabunge au mbunge yeyote akifukuzwa chama chake. Vinginevyo anaweza kushitakiwa mahakamani kwa kuvunja sheria kuu ambayo ni katiba ya nchi.