Iruru
JF-Expert Member
- Jan 27, 2014
- 1,471
- 2,891
Nimemsikiliza Ndugai akilalamika juu ya ajira zilizotangazwa na hasa akijikita kwenye ajira za ualimu.
Malalamiko yake yako kwenye kamati yake ya bunge kwamba hawafuatilii hizi ajira na namna zinavyopatikana. Hili la ufuatiliaji wa kamati ya bunge ni sawa kabisa.
Ila alienda mbali zaidi na hili ndilo lilinipa ukakasi. Ndugai anataka ajira zizingatie mgawanyo wa kieneo, yaani kila eneo katika nchi lipate uwakilishi sawa katika ajira.
Alitaja mifano michache ya ajira zilizopita kwamba aliangalia na kuona huyu ametokea kule, yule katokea kule na huyu katokea kule. Hoja yake hapa pamoja na kwamba hakutaja eneo wanalilotoka hao aliowataja ni kwamba kuna eneo la nchi hii lilipata wananchi wengi walioajiriwa.
Hoja yangu hapa ni hii, pamoja na kwamba ni sahihi kwamba kila mtu ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayo haki ya kuajiriwa, ila utumishi wa umma hautakiwi kuangalia mtu katoka wapi kama kigezo cha ajira.
Ndugai kama spika wa bunge anatakiwa kujua sheria inavyotaka inapotokea suala la kuajiri. Ni lazima uajiri watu kwa merits zao na sio eneo wanakotokea.
Kwa jicho la husda, ni kama Ndugai yeye ajira zinazopitia kwenye himaya yake kuna watu huwa anawaangalia zaidi wapate ajira na wengine wasipate. Hii ni hatari kwa utumishi wa umma na nchi yetu kwa ujumla.
Mawazo ya kina Ndugai yasipothibitiwa, kuna hatari ya kulidodosha taifa hili hapo mbeleni.