Lord OSAGYEFO
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 3,085
- 4,890
Hakika inashangaza na kustajabisha kwanini spika aliyeapa kuulinda na kuitumikia katiba ya nchi leo ndio anakuwa kiongozi tena wa mhimili anaivunja Katiba kwa makusudi na kuteteta uvunjaji wake wa Katiba na Serikali kupitia Mwanasheria mkuu wa Serikali ipo kimya.
Spika huyo huyo aliwahi kuwafukuza wabunge 8 wa cuf baada ya mwenyekiti wa CUF Prof.Lipumba kumwandikia barua Spika Ndugai ya kumtaarifa juu ya kufukuzwa kwao na kuwaapisha wengine haraka na Spika Ndugai hakudai muhtasari wala katiba ya CUF. Kama haitoshi Spika Ndugai huyo huyo aliwahi kumfukuza mbunge Sophia Simba baada ya chama chake cha CCM kumfukuza uanachama na hatukumsikia Spika Ndugai kudai muhtasari wala Katiba ya CCM je kwanini CHADEMA ndio wanatakiwa kupeleka muhtasari
Na katiba ya chama?
Ni wazi suala hili spika ndugai inawezekana ana maslahi binafsi na hao wabunge fake 19 na ukimya wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na tume ya uchaguzi kutokujibu barua ya CHADEMA kwa miezi 5 sasa na pia kitendo cha DPP kumtoa mmoja wa hao wabunge mahabusu ili akaapishwa vitendo vyote hivyo vinaashiria ni mpango uliopangwa.