Spika Ndugai na Katibu wa Bunge wapelekwe Mahakamani kwa kutoiheshimu Katiba waliyoapa kuitetea

Wivu utakuumiza sana
Let's say bungeni wangekuwa hawapati pesa yoyote ni kazi ya kujitolea sidhan kama ungekuja kulialia hapa
 
Mbona ruzuku hamuachi?
 
Uko sawa, ila niambie hata mishipa ya fahamu hawana kuwa katiba inavunjwa?
Anzeni kwanza chadema kukataa ruzuku inayotoka kwenye serikali ambayo imeingia kwa uonevu Then ndio mje na ishu ya ndugai
 
umesahau hawa miamba wanakinga eeeeeeeeehhh
Hata Rais Chiluba alipostaafu alikuwa na kinga. Lakini aliyefuata alitumia taratibu halali kuiondoa na akashtakiwa na kufia ndani.
Hawa hawatakufa ila cha moto watakiona
 
Wivu utakuumiza sana
Let's say bungeni wangekuwa hawapati pesa yoyote ni kazi ya kujitolea sidhan kama ungekuja kulialia hapa
We kweli mwehu! Kwani kalia au kaeleza?
Halafu sidhani kama Chadema wanashida na wanalipwa nini! Walisha weka wazi kuwa Ndugai awatambue tuu wabunge wake lakini wasiseme wabunge wa Chadema bali awaite apendavyo maana hawana agenda ya chama wanayo iwakilisha pale.
Akae nao na kuwalipa apendavyo, ila bado atakuwa kavunja katiba maana mbunge lazima awe na chama.
Umenielewa brother!
 
Anzeni kwanza chadema kukataa ruzuku inayotoka kwenye serikali ambayo imeingia kwa uonevu Then ndio mje na ishu ya ndugai
Nimewaomba ushahidi wa risiti ya kutoa na kupokea hiyo ruzuku mmeshindwa kuonyesha. Basi inaelekea COVID imewapanda kichwani.
CHADEMA wamekataa hiyo inayoiywa ruzuku inayotokana na uchaguzi haramu.
Ujue mnadanganyana nyie maCCM na propaganda zisizo na mashiko.
 
Umepotoka Sana, nadhani ni kwasababu ya njaa.
Spika alishapelekewa barua kumfahamisha kuwa Hilo kindi limefukuzwa uanachama. ILITOSHA.
Kuwasimamisha, siyo suala la hukumu.
Mcoment huku mkimwogopa Mungu.

Huku mkijua kuwa baada ya maisha haya kuna maisha nje ya ulimwengu huu kwa mujibu was maandiko matakatifu
 
Wamejiwekea sheria ya kulinda maovu yao. Sheria haramu hakuna atakayeiheshimu. Utawala ukija mwingine, watafungwa tu maisha jela
Kama Chadema walivyojiwekea sheria ndani ya Katiba yao kulinda udhalimu wao eti Mwanachama akienda Mahakamani kukishitaki chama basi moja kwa moja uanachama wake unakuwa umekoma
 
Tuna shida kubwa sana kwamba tuna rais asiyejua kwamba kila mtu ktk nchi anapaswa kufuata sheria bila shuruti.

Tatizo Magufuli amejenga tabia ya kiburi na kuamini kua yeye yuko juu ya sheria na kwamba kwa kauli yake anaweza kutengua sheria yoyote iliyomo kwenye katiba ya nchi.

Ndugai yupo kutii chochote kile anachoagizwa na Magufuli kukifanya, atafanya tu na wala kamwe hawezi kuhoji na ndio maana Magufuli alipanga akawapa kinga bandia ya kutokushitakiwa.
 
Mahakama ipi ?
 
Job Ndugai alishasema waziwazi kwamba hakuna mahakama Tanzania inauwezo wa kumsimamisha na kumhoji juu ya jambo lolote lile - Yeye ndiye mwenye uwezo wa kumwita Jaji yoyote yule Bungeni na akachukuliwa hatua za kinidhamu lakini si yeye kwenda the other side
 
Ndugai ndie mbunge ambae daima ni mfano bora wa kuepukwa na jamii, Amelifanya bunge kuwa la kudharauliwa kuliko mabunge yote tangu tupate uhuru! Sidhani kama lina hadhi ya kuitwa bunge!
Kama kuna kifyonza damu kinacho nyonya damu ya watanzania kinguvu ni hili dude tunaloliita bunge.
Kodi zote za waTz zinazolipwa kwa hawa watu ikiwa ni mishahara na posho nene ni wizi wa kutumia nguvu.
Hakuna taasisi iliyojidharaulisha na kwa hivyo kukosa uhalali kwa nchi kama hili bunge la Ndugai.
 
Kama Chadema walivyojiwekea sheria ndani ya Katiba yao kulinda udhalimu wao eti Mwanachama akienda Mahakamani kukishitaki chama basi moja kwa moja uanachama wake unakuwa umekoma
Tunajadiri Nchi, Bunge la nchi. Kesho njoo na hoja ya CDM. Hii ni Ndugai na Bunge la JMT!
 
Niliandika nilivyoelewa hilo suala.Nashukuru mno na hii ina maana hata rufaa yao ikikubaliwa watarudi kuwa wanachama lakini ubunge utakuwa NO kwa mtizamo wa ki CDM.
Asante kunielimisha ila Alhamdullila sina njaa kiasi cha kuandika kitu ambacho sicho ninachoamini na nikihisi panaweza na sababu za "kiusalama"mara nyingi naacha kuandika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…